“Hapa sizungumzii viongozi wa CCM au wa Chadema au chama kingine, nazungumzia viongozi wa nchi watakaoweza kufanyia kazi matatizo ya Watanzania.
“Ni vizuri viongozi wakaandaliwa, isiwe mtu
anaibuka tu anagawa hela halafu anashinda. Anatakiwa mtu atakayeweza
kushughulikia matatizo hayo.
Watanzania ni wapole na wavumilivu lakini wanazungumza. Hivyo anahitajika kiongozi atakayesikiliza mahitaji yao na kutoa suluhisho, si kutoa ahadi za uongo,” alisema.
Dk Salim alisema katika kipindi hiki, anahitajika kiongozi atakayekuwa juu ya tofauti za kisiasa, kidini, asili.

“Unajua hapa nchini kama ilivyo mahali pengine,
ukiingiza mgawanyiko wa kidini wakati familia nyingi zina watu wa dini
tofauti, wote wataathirika.”
Akizungumzia tatizo la rushwa, Dk Salim alisema ni kubwa na kadri linavyoongezeka, linakuwa adui wa uwajibikaji, demokrasia.
Alisema katika enzi za utumishi wake nje ya nchi,
alikuwa akiona rushwa ilivyokithiri katika nchi mbalimbali, lakini hapa
nyumbani pakiwa salama hadi akawa anasema Tanzania ina bahati, kauli
ambayo hawezi kuisema sasa.
Dk Salim alibainisha kuwa uongozi unaoingia
madarakani kwa rushwa hauwezi kuwa mzuri kwa nchi na athari zake
zinaonekana hadi ngazi ya chini katika huduma za jamii kama mahakamani,
polisi na hospitalini.
0 comments:
Post a Comment