HABARI PICHA: VIONGOZI WAKUU WA CHADEMA WATINGA OFISI YA MSAJILI MKUU WA VYAMA VYA SIASA NCHINI TANZANIA!!



 Wanachama na Viongozi wa Chadema wakiwemo wa Baraza Kuu la chama hicho, wakipiga kwata kuelekea Ofisi za Msajili wa Vyama vya Siasa, jijini Dar es Salaam, leo kupeleka barua ya kumuomba Msajili huyo wa vyama, kuwataka viongozi wa ngazi ya juu wa Chadema kuzingatia Katiba ikiwemo kuitisha kikao cha Baraza Kuu na kuzingatia matumizi bora ya fedha za Chama.
 Mjumbe wa Baraza Kuu Chadema ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya Temeke Joseph Yona (kushoto) akiongoza wenzake kuingia Ofisi ya Msajili wa Vyama leo kuwashitaki viongozi wa ngazi ya juu wa chama hicho kwa kudaiwa kutotekeleza Demokrasia na kufuata Katiba ndani ya Chama
 Yona akisaini kitabu cha wageni kwenye kwenye mapokezi ya Ofisi ya Msajili wa Vyama Jijini Dar es Salaam, alipowasili ya ujumbe wake. Kulia kwa Yona ni Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Kaliua mkoani Tabora ambaye ni Mjumbe wa  Baraza Kuu na Mjumbe wa Mkutano Mkuu Chadema, Jorum Mbogo
 Naibu Msajili wa vyama vya Siasa Nchini akimkaribisha Yona na msafara wake.
 Wanachama waliofuatana na wajumbe wa Baraza Kuu Chadema wakisubiri kuwasilisha barua yao kwa Mkuu wa Masijala wa Ofisi ya Msajili wa vyama.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment