Wafanyabiashara
wa Mkoa wa Morogoro wamegoma kufungua maduka leo wakitaka kuonana na
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kwa Lengo la kushinikiza kukataa mashine za
kieletroniki za mamlaka ya mapato tanzania.Wafanya biashara hao wamegoma
kufungua maduka tangu asubuhi wakishinikiza kuonana na mkuu wa mkoa
jambo ambalo Mkuu wa mkoa amekubali na kuwaomba wateuliwe wawakilishi 8
kwa ajili ya kwenda kuonana nao.Baada ya wawakilishi kuteuliwa bado
wafanyabiashara hao walishinikiza kuandamana mpaka nje ya ofisi ya Mkuu
wa Mkoa ndipo Jeshi la Polisi walipoingilia kati .
Jeshi la
Polisi wakiwa barabara inayoelekea Kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa
Morogoro Kulinda Amani na kuzuia maandamano yaliofanywa na
wafanyabiashara hao muda huu.
Waduka yakiwa yamefungwa katikati ya Mji wa Morogoro

0 comments:
Post a Comment