Info@DiraYetu

Thursday, 7 August 2014

MAONYESHO YA NANE NANE JIJINI ARUSHA!!


Ofisa mahusiano wa shirika lisilo la kiserikali la Farm Africa, Goodness Mrema (kushoto) akiangalia uyoga uliohifadhiwa kitaalamu na mkulima wa uyoga wa kijiji cha Bashnet wilayani Babati, Rahabu Manase, kwenye maonyesho ya wakulima nane nane, viwanja vya Themi jijini Arusha jana (katikati) ni Ofisa miradi wa misitu na masoko wa shirika hilo, Hakam Mohamed.
Watanzania wenye asili ya bara la Asia wakinunua mafuta ya ufuta kwenye banda la shirika la Farm Africa, katika maonyesho ya wakulima nane nane kanda ya kaskazini, viwanja vya Themi jijini Arusha jana.
Mtoto wa jijini Arusha akipewa asali alipotembelea banda la shirika la Farm Africa jana kwenye maonyesho ya wakulima nane nane kanda ya kaskazini, yanayofanyika viwanja vya Themi jijini Arusha.
Unknown at 02:23
Share

No comments:

Post a Comment

‹
›
Home
View web version
Powered by Blogger.

About Me

Unknown
View my complete profile