![]() |
Mtoto pekee wa Mwimbaji Whitney Houston Bobby Kristina. |
Bado kuna utata kuhusu kinaachoendelea juu ya afya ya Bobbi Kristina, mtoto wa pekee wa Marehemu Whitney Houston,
mengi yanaendelea kuzungumzwa kuhusu hali yake huku wengine wakisema
kuwa leo ni siku ambayo familia hiyo imeruhusu madaktari kumtoa mashine
ya kupumulia ambayo aliwekewa toka siku ambayo alifikishwa hospitali
baada ya kukutwa akiwa ameanguka ndani ya bafu, Georgia Marekani.
Baada ya yote kusikika familia ya Bobbi imeamua
kutumia kampuni ya wanasheria wao kutoa maelezo rasmi kuhusu kila
ambacho kimesikika juu ya hali ya mtoto huyo, taarifa hiyo imekanusha
uvumi wote uliowahi kusikika ikiwemo ishu ya kumtoa mipira ya kupumulia
siku ya leo ambapo ni siku ambayo mama yake alifariki.
Katika taarifa hiyo ya Wanasheria wa
familia hiyo wamesema wanaangalia namna ya kuwachukulia hatu wote
waliotoa taarifa za uongo ikiwemo waliosema walizungumza na wahusika wa
familia hiyo kitu ambacho sio kweli.
Marehemu Whitney Houston akiwa na mtoto wake Bobbi Kristine wakati akiwa mdogo.
Bobbi Kristina akiwa na Oprah Winfrey
Hautopitwa na story yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza
0 comments:
Post a Comment