Thursday, 12 February 2015

NIGERIA: RAIS AKANA KUCHELEWESHA UCHAGUZI!!

Rais Goodluck Johnathan wa Nigeria
Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan amekana kwamba alishauriwa kuhusu kuahirisha  uchaguzi wa Urais nchini humo siku ya jumamosi.

Maafisa wa uchaguzi walichukua hatua hiyo kufuatia ushauri wa wasiwasi wa maafisa wa usalama kuhusu mashambulizi ya wapiganaji wa Boko Haram kaskazini mashariki alisema.

Kucheleweshwa kwa uchaguzi kwa kipindi cha wiki moja sio kitu kikubwa alisema katika runinga ya taifa hilo la Nigeria.

Upinzani unadai kwamba bwana Johnathan alilazimisha uchaguzi huo kucheleweshwa kwa kuwa alikuwa anaogopa kushindwa.

Uchaguzi huo umeahirishwa hadi 28 mwezi machi.
Wachanganuzi wanasema kuwa uchaguzi huo ndio ulio na ushindani mkali tangu uongozi wa kijeshi ulioisha mwaka 1999.

No comments:

Post a Comment