Suarez aliwashangaza mashabiki wa Man City baada kupachika wavuni mabao yote mawili na hivyo kuwaonyesha ni moto wa kuotea mbali anapofika kwenye kisanduku cha kumi nane.
Goli pekee la kufutia machozi la Manchester City lilitiwa kimiani na mshambuliaji wa timu hiyo Sergio Aguero. Na hivyo hadi mechi hiyo inamalizikia Man City wakiwa nyumbani walijikuta wakivuna juani goli moja dhidi ya magoli mawili ya Barcelona.

Magoli ya Juventus yalitiwa kimiani na Carlos Tevez na Alvaro Morata huku lile la Borussia Dortmund likitiwa kimiani na Marco Reus.

Kindumbwe ndumbe cha michuano hiyo kitaendelea tena hii leo ambapo Arsenal ya England watakuwa na kibarua kigumu dhidi ya Monaco ya Ufaransa huku Bayern Levekuzen wakimenyana vikali na Altetico Madrid ya Hispania. Mechi hizo zote zitapigwa mwendo wa saa 4:45 kwa saa za Afrika Mashariki.
0 comments:
Post a Comment