FA CUP: WEST BROMWICH ALBINO, BLACKBURN ROVERS, READING ZATINGA ROBO FAINALI!!

West Bromwich Albion, Blackburn Rovers na Reading Leo zimetinga Robo Fainali ya FA CUP baada ya kushinda Mechi zao za Raundi ya 5.
 
Kwenye Mechi ya Awali kabisa, WBA, wakicheza Nyumbani The Hawthorns, waliitandika West Ham Bao 4-0 kwa Bao za Brown Ideye, Bao 2, na nyingine za James Morrison na Saido Berahino.

West Ham walimaliza Mechi hii wakiwa Mtu 10 baada ya Morgan Amalfitano kutolewa kwa Kadi Nyekundu katika Dakika ya 70 baada ya Kadi za Njano 2.

Nao Blackburn Rovers, wakiwa kwao Ewood Park, walitoka nyuma kwa Bao la Peter Crouch la Dakika ya 10 na kushinda kwa Bao 4-1 kwa Bao 3 za Joshua King na Penati ya Rudy Gestede ambayo ilitolewa baada ya Geoff Cameron kumwangusha King na kupewa Kadi Nyekundu katika Dakika ya 45.

Huko Pride Park, Wenyeji Derby County walitupwa nje baada ya kuchapwa Bao 2-1 na Reading baada ya kucheza Mtu 10 kuanzia Dakika ya 39 kufuatia Kadi Nyekundu kwa Stephen Warnock baada ya Kadi za Njano mbili.

Licha ya upungufu huo na kutanguliwa kwa Bao la Dakika ya 53 la Hal Robson-Kanu Derby waliweza kusawazisha Dakika ya 63 kwa Bao la Darren Bent lakini Mchezaji mpya wa Reading, Yakubu Aiyegbeni kutoka Nigeria, aliingizwa kutoka Benchi katika Dakika ya 71 kwa Mechi yake ya kwanza kabisa na Dakika ya 82 kufunga Bao la ushindi.

FA CUP MICHEZO ITAKAYOFUATA:
RAUNDI YA 5:
Saa za Bongo
Jumapili Februari 15
1530 Aston Villa v Leicester City
1730 Bradford City v Sunderland
1900 Arsenal v Middlesbrough

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment