Rais Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini. (Picha na Maktaba) |
Rais Jacob Zuma amesema kuwa hakuna Wageni hawatakaoruhusiwa kumiliki ardhi Afrika Kusini, ikiwa ni moja ya sheria kali zinazopendekezwa na Rais Jacob Zuma.
Mbali na hayo, mtu yeyote anayemiliki zaidi ya hekta 12,000 atalazimishwa kuiuzia serikali ili ipate kugawiwa.
Ardhi bado ni swala linalozusha hamasa nchini humo ambako karne tatu za ukoloni na ubaguzi wa rangi - zimeacha ardhi nyingi mikononi mwa wachache, hasa wazungu.
Tangu kumalizika kwa ubaguzi wa rangi mwaka 1994, chama tawala cha ANC, kimeshindwa kufikia lengo lake la kugawa theluthi ya ardhi ya kilimo kwa Waafrika, ulipofika mwaka 2014.
0 comments:
Post a Comment