Ujerumani yakabidhi kambi ya Kunduz,Afghanistan.
Baada ya kipindi cha miaka kumi jeshi la Ujerumani Bundeswehr
Jumapili(06.10.2013) limekamilisha jukumu lake kaskazini mwa Afghanistan
kwa kukabidhi rasmi mamlaka ya kambi yao ya Kunduz kwa vikosi vya
Afghanistan.
Mawaziri wa Ujerumani na Afghanistan wakishuhudia wakati maafisa
waandamizi wa kijeshi wa Ujerumani na Afghanistan wakisaini nyaraka za
makabidhiano ya kambi ya Kunduz.
Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Thomas de Maiziere na Waziri wa Mambo ya
Nje wa Ujerumani Guido Westerwelle kwa pamoja wameikabidhi kambi hiyo
kwa vikosi vya usalama vya Afghanistan katika ziara isiotangazwa
iliofanyika Jumapili wakitokea kwenye kambi ya jeshi la Ujerumani ya
Mazar-i-Sharif. Akizungumza katika hafla hiyo de Maiziere amezungumzia
juu ya kujitolea roho zao kwa wanajeshi wa Ujerumani huko Kunduz ambapo
18 wameuwawa kutokana na mashambulizi na katika mapambano wakati wa
kutimiza majukumu ya Kikosi cha Kimataifa cha Usaidizi (ISAF) chini ya
usimamizi wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO.Amesema "Kwetu sisi Kunduz ni
mahala ambapo Bundeswehr ilipigana kwa mara ya kwanza na ilibidi
kujifunza kupigana.Huo ulikuwa wakati muhimu wa maamuzi sio tu kwa jeshi
la Ujerumani bali pia kwa jamii ya Ujerumani."
Waziri huyo amesema juu ya kwamba jeshi la Ujerumani linaondoka katika
jimbo hilo amesisitiza kwamba katu hawatolisahao kwa kuwa lina umuhimu
mkubwa wa kiishara kwa jeshi la Ujerumani. Amesema Kunduz ni mahala
ambapo imelishughulisha jeshi la Ujerumani kuliko mahala popote
pale,hapo walijenga na kupigana,walilia na kujifariji,waliuwa na
kuuliwa. de Maiziere amesema "Kunduz daima itakuwa sehemu ya kumbukumbu
yetu ya pamoja."
@DW
POSTED BY:
www.info@dirayetu.blogspot.com
No comments:
Post a Comment