Thursday, 14 August 2014

HABARI PICHA: EPHRAHIM KIBONDE, GARDNER HABASH HATIANI!!

MTANGAZAJI wa Clouds FM, Ephraim Kibonde na mwenzake, Gardner Habash wa Times FM leo wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya Kinondoni jijini Dar es Salaam kwa kusababisha ajali na kudharau amri ya polisi na kutoa lugha ya matusi.
Watangazaji hao wamesomewa mashitaka hayo na Wakili wa Serikali, Salim Mohammed mbele ya Hakimu Aniseta Wambura.
Kesi yao imeahirishwa mpaka Septemba 10 mwaka huu itakaposikilizwa tena.

No comments:

Post a Comment