Askari wa Kikosi cha zimamoto na Uokoaji wakizima moto uliokuwa unawaka
katika mitambo ya kuzalisha umeme ya songas, Ubungo jijini Dar es Salaam jana.Picha na Francis Dande
---
Mitambo ya kuzalisha umeme ya Songas iliyopo Ubungo jijini dar es Salaam, usiku wa kuamkia jana imeungua moto kabla ya kudhibitiwa na Kikosi cha Uokoaji na Zimamoto kwa kushirikiana
na kikosi cha Kampuni ya Knight Support.
Akizungumzia
tukio hilo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco), Mhandisi
Felichesim Mramba, alisema hitilafu hiyo imetokea katika kituo cha 33kv na
kusababisha gridi ya taifa inayotumika jijini Dar es Salaam kuzimika, hivyo
baadhi ya maeneo umeme ukawa umekatika.
“Tulipata
taarifa saa 10 kuwa kuna hitilafu hapa na tukajaribu kuwasiliana na Idara ya Zimamoto
kwa simu wakawa hawapatikani mpaka tulipowafuata ofisini kwao. Nashukuru baada
ya taarifa walifika kwa wakati na wakafanikiwa kuudhibiti moto,” alisema.
Alisema
kuwa kutokana na hitilafu hiyo maeneo mbalimbali ya jiji yaliyokuwa yakipata
umeme kupitia kituo hicho yataathirika na kuyataja kuwa ni Kigogo, Mburahati,
Magomeni, Tandale na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Meneneo
mengine ni Changanyikeni, Kimara, Tabata na Riverside na kwamba juhudi
zinafanyika kuangalia uwezekano wa maeneo hayo kuunganishwa katika njia
nyingine kwa muda.
Aliongeza
kuwa bado hawajajua thamani halisi ya hasara iliyopatikana na muda utakaotumika
kufanya marekebisho huku akiainisha kuwa ukarabati wa vifaa hivyo unaweza
kuchukua wiki moja mpaka mbili kutegemea na aina ya uharibifu.
Baadhi
ya mashuhuda waliliambia gazeti hili kuwa moshi uliokuwa ukitoka katika mitambo
hiyo ulikuwa mzito na uliwasababishia kushindwa kupumua vizuri.
“Niliwaona
kina mama na watoto waliokuwa wanakwenda katika kituo cha mabasi Ubungo
wakipata taabu kupumua hadi tukawa tunawasaidia kuwapeleka mbali na eneo la
tukio,” alisema Gervas Lutabalize, ofisa wa Chama cha kutetea abiria.
Kamanda
wa Kikosi cha Zima Moto na Uokoaji jijini Dar e s Salaam, ACP Jesward Ikonko,
alisema walipata taarifa ya tukio saa 11:58 alfajiri na kufika katika tukio saa
12:5 ambapo waliwakuta wafanyakazi wa kikosi cha Knight Support wakiwa
wameshaanza kazi ya kuzima moto.
0 comments:
Post a Comment