Kwa mujibu wa taarifa zilizo kwenye
Mtandao wa Reuters, zilisema kuwa fedha hizo zimeongezeka hivyo kwa
kipindi cha kati ya mwaka jana na mwaka huu.
"Ingawa kiasi cha fedha hizo
kimetofautiana kila mwaka kwa mwongo mmoja uliopita," inasema sehemu ya
taarifa hiyo ya Reuters ambayo ilikuwa ikinukuu ripoti za Benki Kuu ya
nchi hiyo.
Hata hivyo, taarifa hizo hazikufafanua ni kwa nini fedha hizo zimeongezeka kwa kiasi hicho.
Taarifa za awali kutoka kwenye kamati ya
Serikali inayochunguza mabilioni hayo, ilionyesha kuwa kuna uwezekano wa
kuwapo kwa fedha nyingi nchini humo kuliko zile zilizotolewa na ripoti
ya benki hiyo ya mwaka 2012 iliyosema kuwa kulikuwa na Dola za Marekani
milioni 3.6.
Taarifa hizo zinasema mbali na fedha kuna
uwezekano mkubwa wa Watanzania kuwa na nyumba na rasilimali nyingine
walizowekeza nchini humo.
Januari 11, mwaka huu, Balozi wa Uswisi
nchini,Olivier Chave, aliliambia gazeti hili katika mahojiano maalumu
kuwa hakuna jitihada zozote zilizofanywa na Serikali ya Tanzania kutaka
ufumbuzi wa tuhuma za watu walioficha fedha nchini humo.
Siku chache baadaye Mwanasheria Mkuu wa
Serikali, Frederick Werema alizungumza na gazeti hili na kusema kuwa
hawezi kumjibu chochote balozi huyo kwa kuwa ni mtu mdogo kwake.
"Najua kuwa huyu balozi ana kinga, ila
siyo adabu hata kidogo kuzungumza maneno yale kwenye nchi ya watu. Kama
ingekuwa ni balozi wa Tanzania huko Uswisi kasema maneno haya,
angeambiwa tu arudi nyumbani kupumzika hadi watakapomhitaji," alisema
Werema.
Werema alisema kwenye Bunge lililokaa Aprili mwaka huu wangekuwa na kitu cha kuwasilisha bungenijambo ambalo halikutimizwa.
Baada ya ukimya huo, Mbunge wa Kigoma
Kaskazini, Zitto Kabwe, alimwandikia Katibu wa Bunge barua akitaka
Serikali iwasilishe majibu juu ya uchunguzi wa fedha hizo kwenye Bunge
lijalo.
Gazeti hili lilipomtafuta Katibu wa
Bunge, Dk Thomas Kashililah ili kujua kama amepata barua hiyo alisema
kuwa "Mimi sijaipokea hiyo barua na nimetoka ofisini leo saa kumi na
sikuiona, labda kama alimtuma mtu na amekaa nayo."
Kwa upande wake Zitto alisisitiza kuwa
"Hiyo barua nimeipeleka leo (jana) saa tano na kawaida tunazipeleka
masijala ndiyo wampelekee, hatumpi katibu mkononi moja kwa moja."
0 comments:
Post a Comment