BARAZA la Habari Tanzania ( MCT) kwa kushirikiana na Baraza la Elimu ya Ufundi (NACTE), hayatakubali kuona viwango cha ufundishaji wa Vyuo vya Uandishi wa Habari nchini katika kutumia mtaala mpya ya taifa yenye ithibati ya Nacte unakwamishwa.
Katibu
Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania, Kajubi Mukajanga, alibainisha
hayo juzi mjini hapa wakati akifungua mafunzo ya matumizi ya mtaala mpya
kwa baadhi ya Walimu wa Vyuo zaidi ya tisa vya Uandishi wa Habari
nchini , mafunzo yaliyopangwa kumalizika jana (sept 27), mkoani hapa.
Kwa
mujibu wa Katibu Mtendaji wa MCT, mtaala huo utatumiwa kufundishia
wanafunzi wa uandishi wa habari ngazi ya cheti na diploma yaani ngazi za
kiufundi za nne , tano na sita ambapo lengo ni kuweka ubora wa taaluma
hiyo katika vyuo vya Uandishi wa habari nchini.
“
Vyuo vya Uandishi wa Habari Tanzania vinakatiwa vifikiee katika ngazi
ya juu ya ubora kwa cheti na diploma ...kada hii ndio waaandishi wazuri
wa habari , hivyo ni muhimu sana kujenga ubora huo kwa kuwa na mtaala
mmoja wa kitaifa” alisema Mukajanga
Alisema
, mtaala huo ni wa Vyuo vya Uandishi wa Habari na kwamba NACTE pamoja
na MCT watasaidia kuboresha na kuhakikisha unatumiwa kufundishia kwenye
Vyuo hivyo.
Hata hivyo alisema, haitoshi kujua kuandika ‘intro’ na baadaye ukajiita ni mwalimu , bali mwalimu ni zaidi ya kujua kitu cha ziada kwa ajili ya kuwafundisha wanafunzi.
Kwa
mujibu wa Katibu Mtendaji huo mapema mwakani , NACTE na Baraza hilo
watafanya mapitio ya mtaala huo ili kuangalia mapugufu kwa lengo la
kufanya maboresho zaidi.
Pia alisema , MCT itapo katika mchakato kukutana na wamiliki wa Vyombo vya Habari nchini ili kupata maoni yao yatakayoweza kufanikisha kuboresha sekta ya Habari nchini.
About Unknown
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment