Mwakyembe abaini kutobolewa kwa bomba la mafuta bandarini....Atoa siku 2.



Waziri wa uchukuzi Dkt. Harrisoni Mwakyembe amebainisha wizi wa mafuta katika bomba la mafuta eneo la mjimwema Kigamboni na kuagiza askari wasimamizi wa bandari ya Tanzania kuwakilisha majina ya wahusika ndani ya siku mbili.

Mwakyembe ameyasema hayo wakati akizungumza na wafanyakazi wa mamlaka ya usimamizi wa bandari Tanzania (TPA) na kulaani kitendo cha baadhi ya watu kutoboa bomba hilo na kuunganishia mabomba yao madogo na kuyafungia  maputo yenye uwezo wa kubeba mafuta kati ya lita 16-18 kinyume cha sheria na kukiita kitendo hicho ni kuhujumu uchumi wa nchi ambapo ameishutumu kampuni ya ulinzi ya TIPA kuhusika na kitendo hicho na kuwataka kumpa picha za wafanyakazi wote waliokuwa kitengo cha ulinzi na kama hawatafanya hivyo kampuni hiyo italipishwa fidia.

Naye kaimu mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya usimamizi wa bandari Tanzania Mhandisi Madeni Kipande wakati akijibu mapendekezo yaliyotolewa na waziri Mwakyembe kuhusu wafanyakazi wa mamalaka hiyo amesema kuwa wafanyakazi waliokuwa wameajiriwa kama vibarua watapewa ajira za kudumu na kubainisha kuongezewa posho wafanyakazi hao kutoka laki moja za awali hadi kufikia laki mbili pamoja na laki moja na nusu kama ghrama za chakula.


@ITV
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment