NI KIMBEMBE: CHELSEA vs MAN CITY JUMAMOSI STAMFORD BRIDGE!!


CHELSEAv CITY-SAT-JAN31-SSKatika viwanja vya STAMFORD BRIDGE, Jumamosi hii kutakuwa na Mechi kali na ngumu na ambayo itatoa mwelekeo wa mbio za Ubingwa za Msimu huu wa Ligi Kuu England wakati Vinara wa Ligi hiyo, Chelsea, watakapowavaa Mabingwa wa Ligi hiyo Manchester City.
Huku kila Timu ikiwa imebakiwa na Mechi 16, Chelsea wanaongoza Ligi wakiwa na Pointi 5 mbele ya Man City.

 Mbali ya umuhimu wa kila Timu kupata ushindi, Mechi hii pia inakutanisha Mameneja ambao hawana uswahiba wowote kati yao.

Jose Mourinho na Manuel Pellegrini ni Watu wenye haiba tofauti.

Wakati Jose Mourinho Raia wa Ureno, ni Mtu mwepesi kuchokoza na kubatukia Watu, Manuel Pellegrini, Raia wa Chile, ni Mtu asietingishika na si wa mzaha.

Hawa Wawili walianza kusuguana tangu walipokuwa huko Spain na wote kushika wadhifa wa kuiongoza Real Madrid huku Pellegrini akitangulia na kisha kuondolewa na kujiunga na Malaga na nafasi yake kuchukuliwa na Mourinho.

Wakati Pellegrini anaondoka Real na Mourinho kutinga Real, Mreno huyo alisema: 
“Ikitokea Real ikanifukuza mimi, siwezi kwenda Malaga. Nitakwenda Timu kubwa Italy au England!”alisema.

Msimu uliopita, kwenye Mechi kama hii Uwanjani Stamford Bridge, Fernando Torres ndie aliefunga Bao la ushindi mwishoni na kumfanya Mourinho aruke kwa Mashabiki na Pellegrini kukataa kumpa mkono Mourinho mwishoni mwa Mechi hiyo.

Hata hivyo, licha ya Chelsea kushinda Mechi hiyo, Ubingwa ulienda kwa Pellegrini na City yake, ambayo pia ilitwaa Capital One Cup, na Mourinho kutoka mikono mitupu Msimu huo.

Mechi hii ya Jumamosi inakuja huku kila Timu ikiwa inawakosa Mastaa wao kadhaa na hilo huenda likaleta matokeo tofauti kwenye Mechi hii.

Timu Chelsea ina uwezekano mkubwa wa kuwakosa Majeruhi Cesc Fabregas na Filipe Luis ambao walipata maumivu Jumanne kwenye Mechi ya Marudiano ya Capital One Cup na pia Straika wao mkubwa Diego Costa ambae ameshitakiwa na FA kwa kumtimba Mpinzani wake kwenye Mechi hiyo hiyo na uamuzi wa Adhabu utatoka Ijumaa.

Aidha Man City ambao hawajashinda kwenye Ligi tangu Januari Mosi, wana tatizo kubwa la kumkosa Yaya Toure ambae ndie mhimili wao mkubwa na akikosekana tu Timu hiyo huyumba.

Hivi sasa Toure yupo huko Nchini Equatorial Guinea akiiwakilisha Nchi yake Ivory Coast kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2015.

LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
**Saa za Bongo
Jumamosi Januari 31
1545 Hull v Newcastle               
1800 Crystal Palace v Everton             
1800 Liverpool v West Ham                
1800 Man United v Leicester               
1800 Stoke v QPR           
1800 Sunderland v Burnley        
1800 West Brom v Tottenham             
2030 Chelsea v Man City           
Jumapili Januari 18
1630 Arsenal v Aston Villa         
1900 Southampton v Swansea 
           
MSIMAMO:
TEBO-BPL-JAN25
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment