MAHAKAMA
MKOANI MBEYA IMEWASOMEA MASHITAKA LAURENT NICHOLAUS
KASWAGA(38) MKULIMA NA MKAZI WA KIJIJI CHA IBURA KIWIRA PAMOJA NA WENZAKE 33 BAADA YA
KULA NJAMA NA PAMOJA NA KUFANYA FUJO.
WATUHUMIWA HAO WAMESOMEWA MASHTAKA HAYO NA MWENDESHA MASHTAKA WA POLISI F.3644 D/C JOEL MBELE YA HAKIMU WA MAHAKAMA HIYO MHE.
MEBO MALAKASUKA.
KATIKA SHAURI HILO LA JINAI NO. 169/2013 WASHTAKIWA WOTE WAMEPELEKWA RUMANDE HADI TAREHE 09.10.2013 AMBAPO UAMUZI WA KUPEWA
AU KUTOPEWA DHAMANA UTATOLEWA MAHAKAMANI HAPO.
AWALI IMESEMEKANA KUWA MNAMO
TAREHE 24.09.2013 MAJIRA KATI
YA SAA KUMI NA MBILI ZA JIONI HADI SAA
NNE USIKU HUKO KATIKA KATA YA KIWIRA VITONGOJI VYA KIBUMBE, MPANDAPANDA, KIWIRA – KATI NA KARASHA
WILAYA YA RUNGWE MKOA WA MBEYA. KUNDI
LA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA
SHERIA MKONONI WALIFANYA FUJO KWA KUFUNGA BARABARA KUU YA MBEYA/TUKUYU
WAKITUMIA MAWE MAKUBWA NA MAGOGO ILI MAGARI YASIPITE NA
KUSABABISHA USUMBUFU KWA WATUMIAJI WENGINE WA BARABARA HIYO. THAMANI HALISI
YA UHARIBIFU ULIOTOKEA BADO
KUFAHAMIKA.
HATA HIVYO KATIKA TUKIO HILO GARI T.335 CBE AINA YA
TOYOTA L/CRUISER LIKITOKEA
MBEYA MJINI KUELEKEA TUKUYU LIKIWA LIMEBEBA MIILI YA MAREHEMU WATATU
LILIGONGA MAWE YALIYOKUWA YAMEWEKWA BARABARANI NA WATU HAO KISHA KULIGONGA GARI T. 771 BBE AINA YA TOYOTA
COASTER NA KUSABABISHA MAJERUHI KWA WATU
WAWILI NA UHARIBIFU KWA MAGARI
YOTE MAWILI.
HATAHIVYO CHANZO CHA VURUGU HIZO KIMEDAIWA KUWA NI NYONGEZA YA USHURU WA MAZAO YA NDIZI ZILIZOKUWA ZIKITOZWA TSHS 100/=KWA KILA MKUNGU HADI KUFIKIA TSHS 200/= JAMBO LILILOSABABISHA VURUGU HIZO WAKISHINIKIZA KURUDISHWA KWA
USHURU WA ZAMANI NA KUFUTIWA HUU WA SASA
HATA HIVYO KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI
DIWANI ATHUMANI AMESEMA "CHANGAMOTO KATIKA JAMII
HAZIWEZI KUTATULIWA KWA KUWEKA MAGOGO NA MAWE BARABARANI BADALA YAKE WATAFUTE
UFUMBUZI KWA KUWASILISHA MATATIZO,KERO, NA MAONI YAO KATIKA
MAMLAKA HUSIKA NA KUKAA MEZANI KWA MAZUNGUMZO ILI KUPATA UFUMBUZI
KWA KUZINGATIA HOJA".
AIDHA
AMESISISTIZA KUWA KUFUNGA BARABARA KUNALETA MADHARA KWA WATUMIAJI WENGINE WAKIWEMO WAGONJWA, WASAFIRI, WAGENI KUTOKA MATAIFA MBALIMBALI PIA
KUSAFIRISHA MAITI KAMA ILIVYOTOKEA KATIKA GARI T.335 CBE NA KWAMBA JESHI LA
POLISI KAMWE HALITASITA KUWACHUKULIA HATUA ZA KISHERIA WATU AU VIKUNDI VYA WATU
WATAKAOSABABISHA UVUNJIFU WA
AMANI. |
0 comments:
Post a Comment