KAMPUNI YA MAZIWA YA ASAS DAIRIES LTD YAWANYWESHA MAZIWA WANAFUNZI 30,000 IRINGA.

E84A1958_92552.png
Mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya unywaji maziwa mashuleni mkuu wa wilaya ya Kilolo Bw Gelard Guninita (mwenye koti jeusi kushoto) akiwa na mkurugenzi wa kiwanda cha maziwa cha Asas Dairies Ltd Bw Fuad Asas Abri ,wakiongoza wanafunzi zaidi ya 30,000 wa shule za msingi Manispaa ya Iringa kunywa maziwa fresh.www.info@Dira Yetu.blogspot.com
E84A1743_1_0a292.png

Kampuni ya maziwa ya Asas Dairies Limited leo imetoa msaada wa madawati yenye thamani ya zaidi ya Tsh milioni 2.7 kwa shule za msingi tatu ambazo zimeshinda katika mashindano ya uchoraji wa picha zinazoelezea umuhimu wa unywaji maziwa mashuleni.

Mbali ya zawadi hizo kwa shule hizo tatu pia kampuni hiyo imewanywesha maziwa wanafunzi 30,000 wa shule za msingi katika Manispaa ya Iringa.
Shule hizo zilizopatiwa msaada wa madawati ni pamoja na Hoho iliyoshika nafasi ya kwanza na kupata madawati yenye thamani ya Tsh milioni 1 ,Mlangali iliyoshika nafasi ya pili na kupata madawati ya Tsh.750,000 pamoja na St Dominic iliyopata madawati yenye thamani ya Tsh 500,000.
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo ya maziwa ya Asas Dairies Ltd Bw Fuad Abri alisema kuwa maadhimisha ya mwaka huu yamelenga zaidi vijana hasa wanafunzi wa shule za msingi mjini Iringa.
Alisema kuwa kampuni hiyo inaamini kuwa iwapo shule zitaweka utaratibu wa kutoa maziwa kwa wanafunzi afya za wanafunzi hao zitakuwa bora na kiwango cha elimu kinaweza kuongezeka zaidi mashuleni.
Mbali ya unywaji wa maziwa kuhamasishwa zaidi mashuleni bado viongozi wa serikali wanapaswa kuanza kuhamasha unywaji wa maziwa katika ofisi hizo za umma badala ya kutumia maziwa kutoka nje ya nje.
"uwezekano wa kupata ufadhili kutoka sekta binafsi na taasisi za kimataifa ....ili kutekeleza mpango mkakati utakao hakikisha maziwa yanapatikana mashuleni kwani hilo linalotekelezeka"
Alisema kuwa kampuni ya Asas Dairies
Ltd ipo tayari kushirikiana na wadau wote katika kufanikisha jitihada hizo .

Aidha alisema kuwa kuwa mbali ya kampuni yake kuendelea kuhamasisha unywaji wa maziwa bado itahakikisha inaunda mpango mkakati wa kuhamasisha unywaji wa maziwa kama njia ya kuendeleza kauli mbiu ya mwaka huu ya KUNYWA MAZIWA SHULENI KILA SIKU NI HAKI YA KILA MWANAFUNZI
Kwa upande wake mgeni rasmi katika maadhimisho yao mkuu wa mkoa wa Iringa Dr Christine Ishengoma aliyewakilishwa na mkuu wa wilaya ya Kilolo Bw Gelard Guninita alisema kuwa kuwa mkoa wa Iringa unazalisha maziwa zaidi ya lita milioni 14 kwa mwaka ila bado kiwanda cha asas kinasindika lita 400,000 pekee kwa siku .
Hata hivyo alisema suala la lishe bado ni kikwazo katika mkoa wa Iringa baada ya mkoa huo kuwa mkoa wa pili kwa utapiamlo kitaifa .
Hivyo alitaka jamii ya wakazi wa mkoa wa Iringa kujenga utamaduni wa kutumia maziwa ili kuongeza lishe na kuwa na afya njema.
Alisema kuwa mkoa wa Iringa umejipanga kuendelea kuboresha upatikanaji wa maziwa mashuleni kwa kushirikisha wafugaji kama njia ya kukomesha utapiamlo mkubwa mashuleni.
Kwani alisema kuwa mkoa wa Iringa unapaswa kuondokana na aibu ya utapiamlo kwa watoto na kuwataka wananchi sasa kuanza kuongeza ufugaji wa ng'ombe za maziwa kupitia mradi wa kopa ng'ombe lipa ng'ombe.
Hata hivyo alipongeza jitihada za kampuni ya maziwa ya Asas kwa kuendelea kuhamasisha unywaji wa maziwa na kuitaka jamii na mkoa wa Iringa kuachana na unywaji wa pombe na badala yake kunywa maziwa zaidi.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment