INJINIA ANGELINA MADETE: UKAME UMEKUWA TATIZO KUBWA SANA KATIKA NCHI ZINAZOENDELEA IKIWAMO TANZANIA!!


Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Injinia  Angelina Madete  amesema ukame umekuwa tatizo kubwa sana katika nchi zinazoendelea ikiwamo Tanzania. Na pia umeleta athari sana katika swala zima la mazingira, ameongeza   kuwa katika Africa inakadiriwa aslimia 73 ya nchi imepunguza uwezo wa kuzalisha chakula na hii imepelekea kuongezeka kwa ukame  na hivyo kupelekea upungufu wa chakula Nchini.  Alitaja baadhi ya mikoa iliyoathiriwa na ukame ambayo ni Dodoma, Singida na maeneo machache ya mikoa ya Shinyanga,Mara, Iringa, Manyara na Arusha.
 Amesema hayo leo mjini Bagamoyo  wakati wa  ufunguzi wa warsha ya  siku mbili kuhusu  juu ya   kuenea kwa hali ya jangwa na ukame wa maendeleo endelevu ya ardhi. Warsha hiyo  imewashhirikisha wafanyakazi kutoka wizara mbalimbali za Serikali kwa lengo la kuwaongezea uelewa juu ya umuhimu wa utunzaji wa mazingira kwa lengo  kuepuka  janga la ukame..
Akiongea katika warsha hiyo Injinia Madete alisema  kuwa ukame unaleta umaskini na pia ukame umechangia wananchi wengi kuhama maeneo yao na kwenda sehemu zingine zisizo na ukame. Aliendelea kusema kuwa Serikali imechukua hatua mbalimbali kukabiliana na swala hilo la ukame amabapo mwaka 1994 ilisaini Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Kupamabana na kuenea kwa hali ya jangwa na ukame(United Nations Convetion to Combat Dessertification UNCCD)  na pia serikali inatekeleza mkataba huo kupitia Programu ya Taifa ya kupambana na kuenea kwa hali ya Jangwa na ukame(Nationala Action Programme to Combat Dessertification-NAP). Na kususdi kubwa la mkataba huu ni kuimarisha maisha ya kila siku ya mwananchi wa kawaida aishiye kwenye sehemu za Ukame.
Warsha hiyo ya siku mbili imewashirikisha pia wadau wa mazingira kutoka sehemu mbalimbali wakiwemo wafadhili kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja Wa Mataifa (UNDP)
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment