ROY HODGSON ASEMA: “HARRY KANE YU TAYARI ENGLAND, ROONEY NI MAHIRI AWEZA KUCHEZA HATA FULBEKI!”


MENEJA wa England Roy Hodgson ameweka bayana kuwa Straika Chipukizi wa Tottenham Hotspur, Harry Kane, yupo tayari kuichezea England kwa mara ya kwanza.
 
Kane, mwenye Miaka 21 na ambae alianzia Chuo cha Soka cha Tottenham, Msimu huu ameibuka na kulivuruga Soka la England kwa umahiri wake kwa kutandika Bao 23 kwa Mechi 35 zikiwemo Bao 2 katika kila Mechi dhidi ya Chelsea na Arsenal.

Roy Hodgson, ambae anatarajiwa kukitangaza Kikosi cha England kwa ajili ya Mechi za Makundi za EURO 2016 Mwezi ujao, akihojiwa na Wanahabari, ametamka: 

“Je yeye Kane anastahili kuwemo Kikosini? Ni wazi anastahili! Tushawatumia Wachezaji wengi Vijana. Tulikuwa nae Saido Berahino katika Kikosi kilichopita. Ni wazi anastahili nafasi!”HARRYKANE
Aliongeza: “Kama swali lako ni kwamba anastahili kupewa namba kupita Wayne Rooney, Danny Welbeck na Daniel Sturridge, au yeyote, hicho ni kitu lazima yeye aonyeshe! Lakini bila kumpa nafasi, hatapata nafasi kuonyesha hilo!”

Lakini alipogusiwa kuhusu kuwa na Mafowadi wengi na nafasi ya Kepteni wake Wayne Rooney, ambae ndie Mfungaji Bora wa 3 katika Historia ya England akiwa na Bao 49, kurudishwa kucheza kama Kiungo, Roy Hodgson alieleza: “Rooney ni Mchezaji wa aina hiyo. Anaweza kucheza kokote. Hutanishangaza kama Siku moja akacheza kama Fulbeki na kufanya vyema. Yeye ni Mchezaji mzuri mno!”

Hata hivyo, Roy Hodgson, alisema wao kama England hawamchukulii Rooney kama Mchezaji wa Kiungo kama vile Meneja wake wa Manchester United, Louis van Gaal, anavyomtumia hivi sasa.

Hodgson alisema: “Sisi tunamtumia pozisheni ambayo anaisaidia Timu na sidhani hiyo ni Kiungo kama Man United ambao labda wanao Wachezaji wengine na wanaona katikati ndio anafanya kazi njema. Naheshimu hilo. Lakini yeye ni Mfungaji Mabao, yeye ndie Mfungaji wetu bora, na tunategemea ataendelea kufunga!”

Mechi ijayo kwa England ni Mechi ya Kundi lao la kufuzu kucheza EURO 2016, Kombe la Mataifa ya Ulaya, hapo Machi 27 dhidi ya Lithuania na kisha Siku 4 baadae watatua Turin kucheza na Wenyeji wao Italy katika Mechi ya Kirafiki.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment