Umoja
wa katiba ya wananchi(UKAWA) umesababisha mjumbe wa bunge maalum la
katiba ambaye pia ni katibu wa chipukizi taifa wa chama cha mapinduzi
Paul Makonda kupata wakati mgumu akijaribu kufuta nyayo za UKAWA baada ya kuzomewa
na wananchi na kuondoka katika mkutano wakimuacha jukwaani akishindwa
kuhutubia mkutano huo alipopanda kujibu swali kuhusu katiba mpya.
Nukuu
ya Nyerere ilitumika kumdhoofisha na kushindwa kuhutubia mkutano hadi
ukavunjika huku wananchi wa mjini Geita wakiwaomba Ukawa waendelee
kuwaelimisha wananchi kuheshimu maoni ya jaji Warioba na kuacha
kuwahadaa wananchi kama ambavyo chama cha mapinduzi kimewahadaa katika mkutano huo.
Tukio hilo lilitokea jana katika mkutano wa hadhara wa chama cha Mapinduzi uliofanyika katika viwanja vya soko kuu wilayani Geita ikiwa ni mwendelezo wa chama hicho kushawishi wananchi kuhusu muundo wa serikali mbili katika katiba mpya kama ccm inavyopendekeza.
Baada ya
mwenyekiti wa ccm mkoa wa Geita Joseph Musukuma kumaliza kuhutubia
wananchi,aliomba wananchi kumi waulize maswali ili ayapatie
majibu,ambapo kijana mmoja ambaye hakujitambulisha jina lake,aliuliza swali lililoonekana kuwakera viongozi wa chama hicho na kumfukuza aondoke mbele ya jukwaa .
Kabla ya kuuliza swali kijana huyo alisema........
“Mheshimiwa
mwenyekiti wa mkoa,Jaji Warioba na timu yake ya mabadiliko ya katiba
walizunguka nchi nzima wanakusanya maoni yetu na ndiyo yaliyo andikwa
kwenye rasmu,hata hivyo, baba wa taifa Julius Nyerere aliwahi kusema kwamba,kama kuna watu wanao dhani katiba mpya haitungwi na wananchi basi watu hao ni wapumbavu”.
Kabla hajamaliza kuuliza swali hilo,Katibu mwenezi wa ccm mkoa wa Geita Said Kalidushi
alimnyang’anya kipaza sauti kijana huyo na kumfukuza aondoke huku watu
wakizomea kama ishara ya kupinga kinachofanywa na kiongozi huyo.
Baada
ya mwenyekiti kugundua kuwa wananchi hawakufurahishwa na kitendo
hicho,alipopanda jukwaani kujibu maswali alilazimika kumuita tena kijana
huyo aendelee kuuliza swali hilo huku akiomba swali lijibiwe na Pul
Makonda.
“Baba wa taifa Julius Nyerere aliwahi kusema kuwa ,wale wanaodhani katiba mpya haitungwi na wananchi ,basi watu
hao ni wapumbavu,na nyie ccm mnapinga maoni ya wananchi tuliyotoa kwa
Tume ya Warioba,...swali langu ni je,na nyie ccm ni wapumbavu kama
alivyosema baba wa taifa? maana nyie mnakataa maoni yetu na mnasema
katiba haitungwi na wananchi ila inatungwa na bunge la katiba”?
Baada
ya swali hilo, umati wa mkutano huo ulilipuka kwa kuzomea na
kumshangilia kijana huyo kuashiria kuwa wamekubaliana na alichouliza
kijana huyo.
Mjumbe
wa bunge maalum la katiba ambaye pia ni katibu wa chipukizi taifa wa
chama cha mapinduzi Paul Makonda alipopanda jukwaani kujibu swali,
ghafla wananchi walianza kuzomea na kuondoka katika mkutano huo huku Makonda akipigwa na butwaa na kushindwa kuendelee kuhutubia na kulazimika kushuka jukwaa bila kutoa majibu ya swali hilo.
Tukio
hilo lilitafsiriwa kama ni ishara kwamba watu wengi waliokuwepo katika
mkutano huo pamoja na kwamba uliitishwa na ccm lakini wanapenda muundo wa serikali tatu katika katiba mpya ijayo.
Mkutano huo wa ccm ulilenga kufuta nyayo za mikutano iliyofanywa na viongozi wa umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) iliyofanyika mwezi jana katika mkoa wa Geita ikiongozwa na Dr. Wilbroad Slaa
0 comments:
Post a Comment