Afisa
Habari toka Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa
Umma Kassim Nyaki (KULIA)akieleza kwa waandishi wa habari juu ya
Utekelezaji wa Mchakato wa Ajira katika Utumishi wa Umma wakati wa
mkutano katika ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO).Kushoto ni Katibu
Msaidizi wa Idara ya Ajira toka Ofisi hiyo Bi. Aurelia Matagi.
--
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
Jukumu
kubwa na la Msingi la Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni
kuendesha mchakato wa ajira Serikalini. Tangu kuanza kwa majukumu yake
Machi, 2010 hadi Juni,2013 imetangaza jumla ya nafasi za kazi zipatazo
8,535 ambapo jumla ya maombi 172, 936 yalipokelewa. Kati ya hizo nafasi
5,037 hadi kufikia mwezi Agosti, 2013 zilikuwa tayari zimejazwa na
nafasi 2,291 ujazaji wake upo katika hatua mbalimbali.
Ujazaji
huo umenyumbulishwa kwa jinsi na ngazi mbalimbali za elimu. Kati ya
nafasi 5,037 wanaume walikuwa 2,836 sawa na asilimia 56.3%na wanawake
walikuwa 2,201 sawa na asilimia 43.7%. Wahitimu kutoka Vyuo vikuu ni
2,749 vyuo vya kati 1,999 na wahitimu wa kidato cha nne (4) na sita(6)
(supporting staff) ni 289.
Aidha
kwa mwezi huu wa Septemba,2013 jumla ya waombaji kazi wapatao 949
waliofanya usaili mwezi Agosti wamepangiwa vituo vya kazi na wakati
wowote majina yao yatawekwa kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira.
Baada ya zoezi hili kukamilika tutakuwa tumewashatuma kwa waajiri
waombaji kazi 5,986 na kubakia na nafasi 1,342 ambazo ujazaji wake upo
katika hatua mbalimbali za utekelezaji.
Suala
la pili ambalo ningependa kuliongelea ni upangaji wa wahitimu
wanaokwenda kufanya kazi katika maeneo ya pembezoni. Kwa muda mrefu sana
mikoa iliyopo pembezoni mwa Nchi yetu ilikosa watumishi wa kutosha
kutokana na vijana wengi wenye sifa waliokuwa wakipangwa kutopenda kufanya
kazi katika maeneo hayo. Miaka ya hivi karibuni Serikali imeboresha
miundombinu pamoja na kuharakisha kwa upatikanaji wa huduma muhimu na za msingi katika maeneo mengi nchini.
Uboreshaji
huo wa mazingira ya kazi pamoja na uhaba wa ajira nchini kumeongeza
mwamko kwa waombaji wengi wa fursa za ajira kupenda kufanya kazi katika
maeneo hayo ikiwemo Mikoa ya Mtwara, Lindi, Kigoma na Rukwa. Kwa mfano
tangu kuanza kwa sekretarieti ya Ajira mkoa wa Mtwara tumepeleka
watumishi wapya 234, Lindi watumishi 201, Kigoma watumishi 96 na Rukwa
na Katavi watumishi 122. Mwamko
wa waombaji wengi sasa hivi kupenda kufanya kazi serikalini
unajidhihirisha si tu kwa Sekretarieti ya Ajira kupokea maombi mengi
kila inapotangaza nafasi wazi za kazi bali pia kwa idadi kubwa ya wadau
wanaotembelea Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira. Tangu kuanzishwa kwake
Aprili 2012 hadi kufikia jana imetembelewa na wadau zaidi ya 3,760,000.
Jambo
la tatu ambalo ningependa kuzungumzia ni kuhusu utumaji wa maombi ya
kazi kwa njia ya mtandao (e-application).Kutokana na changamoto nyingi
zinazoendelea kujitokeza kwenye soko la ajira ikiwemo wingi wa waombaji
ambao unaleta ushindani mkubwa, ubora wa wahitimu na ukubwa wa eneo la
Nchi yetu kijiografia, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
inatarajia kufanya mabadiliko kwenye utaratibu mzima wa mchakato wa
ajira nchini ikiwemo utumaji wa maombi ya kazi kwa njia ya Kielectroniki
(e-application). Mfumo huu mpya utawawezesha waombaji wa fursa za
ajira kuwasilisha maombi ya kazi zitakazokuwa zikitangazwa katika
Utumishi wa Umma. Mfumo huo pia unalenga kuboresha mchakato wa ajira ili
waajiri waweze kupata waombaji wenye sifa kwa haraka zaidi.
Kabla
ya kumaliza nitoe wito kwa waombaji wa fursa za ajira ambao bado wana
mtazamo wa kuchagua maeneo ya kufanyia kazi, hususani wale wanaopangiwa
vituo vya kazi na Sekretarieti ya ajira na hawaendi kuripoti bila ya
kutoa sababu za msingi kuwa kwa sasa hawana sababu ya kufanya hivyo kama tulivyoeleza hapo awali na kwa wale wanaofanya hivyo Sekretarieti ya Ajira inaandaa utaratibu wa kutowaruhusu kufanya usaili mwingine.
Imetolewa na Kassim S. Nyaki,
Afisa Habari,
Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
+255-687624975 begin_of_the_skype_highlighting +255-687624975 FREE end_of_the_skype_highlighting.
Facebook page ‘www.facebook.com/Sekretarieti Ajira’.
0 comments:
Post a Comment