Wakati kampeni za kufuzu michuano ya Kombe la Dunia 2014 zikifikia hatua ya mwisho baadhi ya timu mwishoni mwa wiki hii zinaweza kujihakikishia nafasi kushiriki michuano hiyo mwakani.
Wenyeji Brazil tayari wameungana na
wawakilishi kutoka bara la Asia ambao ni Japan, Australia, Iran na Korea Kusini
huku Ulaya tayari kukiwa na vigogo Uholanzi na Italia pamoja na Marekani, Costa
Rica na Argetina.
Katika siku chache zijazo timu
zingine kutoka mataifa ya Afrika, Ulaya, Amerika Kaskazini na Amerika Kusini
nazo pia zinaweza kujihakikishia nafasi katika michuano hiyo.
Kwa upande wa Ulaya nchi za
Ubelgiji, Ujerumani, Switzerland, Urusi, Bosnia-Herzegovina na Hispania
zinaweza kujihakikishia nafasi ya kwenda Brazil kama zikishinda michezo yao ya
Ijumaa.
Wakati Upande wa Amerika Kusini nchi
za Colombia, Chile, Uruguay na Ecuador zote zinaweza kufuzu michuano hiyo kama
wakishinda mechi zao, huku Honduras nao wakiwa na uwezo wa kuwa nchi ya tatu kwa
upande wa Concacaf kufuzu michuano hiyo kama wakiifunga Costa Rica Ijumaa hii.
Wikiendi pia kutakuwa na mechi za
mkondo wa kwanza za mtoano kwa uapnde wa Afrika ambapo Burkina Faso
wataonyeshana kazi na Algeria, Ivory Coast na Senegal, Ethiopia na Nigeria,
Tunisia dhidi ya Cameroon na Ghana wataikaribisha Misri.
POSTED BY:www.info@dirayetu.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment