TRA YATANGAZA VITA NA WATAKAOHAMASISHA MGOMO!!

index
Na Gladness Mushi, Arusha
MAMLAKA ya mapato TRA hapa nchini imetangaza vita kubwa kwa wafanyabiashara wadogo na wakubwa ambao wanashinikiza mgomo wa kufunga biashara kwenye maduka mbalimbali hapa nchini kwa visingizio vya kutotambua matumizi ya mashine za kulipia kodi
Aidha hatua hiyo inakuja wakati wafanyabiashara katika mikoa mbalimbali hapa nchini kufunga maduka na kisha kushinikiza kwa wenzao wasitoe huduma kwa ajili ya kupinga matumizi ya mashine hizo.
 
Akitangaza rasmi vita hiyo ambayo itafanyika katika mikoa yote hapa nchini kaimu  Kamishna mkuu wa mamlaka hiyo Rishedi Bade alisema kuwa serikali kamwe haitaweza kuwafumbia macho wadanganyifu wa biashara ya aina yoyote ile
Alisema kuwa kwa wafanyabiashara wa aina yoyote ile atakayekamatwa kuwa anashinikiza mgomo basi wataweza kuchukuliwa sheria mbalimbali ambazo zitawagarimu kwa kiwango kikubwa sana.
 
Pia aliwataka wafanyabiashara nao kutoingia kwenye mgomo ambao hauwahusu kwani wanajitengenezea harasa zao wenyewe wakati wanaohitajika kutumia mashine hizo za kielekroniki wamebainishwa kwenye sheri
“TRA tunashangaa sana kuona kuwa wafanyabiashara wasiohusika wanafunga biashara wakati wanaohusika ni wengine na kwa hali hiyo tunatangaa vita sasa na wale ambao wanahamasisha mgomo”aliongeza Bade.

Wakati huo huo pia alisema kuwa watakaokamatwa wakiwa wanahasisha mgomo huo hatua watakazochukuliwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani lakini pia hata kuweza kuwafutia leseni zao za biashara
Katika hatua nyingine alisema kuwa matumizi ya mashine hizo ni muhimu sana kwa maendeleo ya taifa la Tanzania kwani zinaweka na kuanisha wazi juu ya mapato halisi ya mfanyabiashara.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment