DR. SHEIN AMPOKEA RAIS WA UJERUMANI MJINI ZANZIBAR LEO!!

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.ALI MOHAMED SHEIN akisalimiana na mgeni wake Rais wa Ujerumani ,JOACHIM GAUCK
Rais wa UJERUMANI - JOACHIM GAUCK anaendelea na ziara yake ya siku Tano hapa nchini kwa mwaliko wa Rais JAKAYA KIKWETE. 

Rais GAUCK amewasili visiwani ZANZIBAR ambapo anafanya mazungumzo rasmi na Rais wa ZANZIBAR na Mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi Dakta ALI MOHAMMED SHEIN kabla ya kushiriki kwenye mkutano wa Kamati ya Pamoja ya Viongozi wa Dini kuhusu Amani. 

Baada ya ziara hiyo huko Zanzibar Rais GAUCK anatarajiwa kwenda jijini ARUSHA kuendelea na ziara yake. 

Pamoja na shughuli nyingine alizozifanya hapo jana, Rais GAUCK, Mkewe Mama DANIELA SCHADT pamoja na ujumbe wake alishiriki katika dhifa ya taifa aliyoandaliwa na Rais KIKWETE katika viwanja vya Ikulu Jijini DSM. 

Akizungumza wakati wa dhifa hiyo Dakta KIKWETE ameishukuru serikali ya UJERUMANI na raia wote wa nchi hiyo kwa misaada yake inayotoa kwa TANZANIA. 

Kwa mujibu wa Rais KIKWETE, misaada hiyo kutoka serikali ya UJERUMANI imekua ikiwasaidia Watanzania katika kuboresha maisha yao. 

Aidha amesema kuwa ushirikiano baina ya TANZANIA na UJERUMANI una faida kubwa kwa pande zote mbili na kuwaomba Wafanyabiashara kutoka nchini UJERUMANI kuja kuwekeza TANZANIA.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment