Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja akitoa maelezo mafupi kuhusu Maendeleo ya Shirika la Magereza kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi ambaye ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Pereira Silima( hayupo pichani) kufungua rasmi Kikao cha Bajeti ya Shirika la Magereza kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014 kinachofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Edema, Mkoani Morogoro.
Naibu
Wazir wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Pereira Silima(Mb) akisoma hotuba
ya ufunguzi wa Kikao cha Bajeti ya Shirika la Magereza ya Mwaka wa
Fedha 2013/2014 kinachofanyika kwa siku mbili kuanzia leo Oktoba 21,
2013 katika Ukumbi wa Edema, Mkoani Morogoro. Baadhi
ya wajumbe wanaoshiriki Kikao cha Bajeti ya Shirika la Magereza kwa
mwaka wa fedha 2013/2014 wakiwemo Wakuu wa Magereza Mikoa yenye miradi
ya Shirika pamoja na Wasimamizi Wakuu wa Miradi hiyo wakisikiliza
hotuba ya Mgeni katika ufunguzi wa Kikao cha Bajeti ya Shirika la
Magereza ambacho kimeanza leo Oktoba 21, 2013 katika Ukumbi wa Edema,
Mkoani Morogoro.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Pereira Silima( wa tatu kulia)
akifuatilia kwa makini uwasilishwaji wa Bajeti ya Shirika la Magereza
kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014 leo Oktoba 21, 2013 katika Ukumbi wa Hoteli
ya Edema, Mkoani Morogoro( kushoto kwake) ni Kamishna Jenerali wa
Magereza Nchini, John Casmir Minja( Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi
la Magereza).
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Pereira Silima((wa tatu kulia)
akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Magereza yenye miradi ya
Shirika mara baada ya kufungua rasmi Kikao cha Bajeti ya Shirika la
Magereza kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014 leo Oktoba 21, 2013 katika Ukumbi
wa Edema, Morogoro( wa tatu kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Magereza
Nchini, John Casmir Minja( wa pili kushoto) ni Kamishna Huduma za
Urekebishaji, Deonice Chamulesile. Wengine ni Kamishna wa Sheria na
Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa( wa pili kulia) na Kamishna wa
Fedha na Utawala, Gaston Sanga( wa kwanza kulia). Picha zote na Lucas
Mboje wa Jeshi la Magereza.
POSTED BY:www.info@dirayetu.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment