RAIS JAKAYA KIKWETE KUZINDUA RASMI MKOA WA NJOMBE OCTOBA16 /2013

rc_2b91c.jpg
Mkuu wa mkoa wa Njombe Kepten Mstaafu Asser Msangi akitoa taarifa ya uzinduzi wa mkoa wa Njombe leo katika ukumbi wa RC
.........................................................................................................................................................................

Serikali mkoa wa Njombe imetangaza ratiba kamili ya uzinduzi wa mkoa mpya wa Njombe ambapo mkoa huo sasa utazinduliwa rasmi na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr Jakaya Mrisho Kikwete Octoba 16 mwaka huu.
Mkuu wa mkoa wa Njombe Kepten Mstaafu Asser Msangi ametoa taarifa hiyo leo katika ukumbi wa RC mjini Makambako kuwa siku ya tarehe 16 mara baada ya Rais Kikwete kutoka mkoa wa Iringa katika kilele cha mbio za mwenge wa Uhuru kitakachomalizika kitaifa mkoani Iringa atafanya uzunduzi wa mkoa huo wa Njombe katika uwanja wa saba saba pamoja na kuweka jiwe la msingi katika ofisi ya Halmashauri ya mji wa Njombe.
Hata hivyo alisema siku inayofuata ambayo ni Octoba 17 mheshimiwa Rais Kikwete atakuwa wilaya ya Makete ambapo shughuli atakazozifanya ni pamoja na kusalimia wananchi wa kijiji cha Kipengere ,kuweka jiwe la msingi sekondari ya Lupalilo,kuweka jiwe la msingi Zahanati ya Ivalalila,kuzindua chuo cha VETA na baadae kuwahotubia wananchi katika mkutano utakaofanyika uwanja wa Iwawa mjini Makete .
Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa Octioba 18 Rais Kikwete atafanya ziara katika eneo la Lupembe Njombe kwa kuzindua kiwanda kipya cha Chai Cha Iganga Tea Company ,kuweka jiwe la msingi mradi wa umeme wa Mapembasi uliopo Halmashauri ya mji .
Wakati Octoba 19 atakuwa wilaya ya Ludewa ambako atazindua maabara ya kisasa katika Hospital ya wilaya ya Ludewa na baada ya hapo atafanya mkutano wa hadhara katika uwanja wa Ludewa mjini .
Katika ziara hiyo wilayani Ludewa Octoba 20 atatembelea mradi wa Liganga(Chuma) katika kijiji cha Mndindi kabla ya kuondoka kuelekea mjini Njombe kwa mapumziko huku Octoba 21 Rais Kikwete atafanya majumuisho ya ziara yake mkoa mpya wa Njombe katika ukumbi wa Halmashauri ya Njombe kabla ya kuondoka mkoani hapo.
Hivyo amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika uzinduzi wa mkoa huo pamoja na maeneo ya miradi ambayo Rais Kikwete atapita mkoani humo.
 @ Francis Godwin Blog Njombe

www.info@dira yetu.blogspot.com 
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment