Sudan mbili zakubali kutatua migogoro.



Sudan Kusini inataka Bashir na AU kuwasikiliza watu wa Abyei kuhusu kutaka kujitawala
Marais wa Sudan na Sudan Kusini wamekubaliana kubuni mikakati ya kusuluhisha maswala yote yanayotatiza uhusiano wa pande hizo mbili.

Viongozi hao walikutana leo wakati wa mkutano wa faragha katika mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba.
Aidha vingozi wa kamati sita wakiwemo, mawaziri kutoka nchi hizo mbili pia walikutana wakati wa mkutano hio na kujadili maswala kuhusu nchi hizo mbili.
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit alielezea furaha yake kwa kufikia makubaliano ya pande hizo mbili akisema kuwa serikali yake itajitolea kuhakikisha kuwa makubaliano hayo yatatekelezwa.
Kwa upande wake Rais Umar al-Bashir alisema kuwa mkutano ulifanikiwa na kuongeza kuwa serikali yake itajitolea kuhakikisha kuwa makubaliano waliyoafikia yanatekelezwa.
Marais hao walifanya mkutano wa faragha muda mfupi baada ya Bashir kuwasili na wajumbe wake wa Sudan katika Ikulu ya Rais mjini Juba.
Kwa mujibu wa shirika la habari la SUNA, baadhi ya maswala yaliyojadiliwa kwenye mkutano huo ni mambo tete kuhusu Abyei,usalama pamoja na kutekelezwa kwa makubaliano ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.
Mnamo siku ya Jumatatu, waziri wa mambo ya nje wa Sudan Kusini Barnaba Marial Benjamin, aliambia kituo cha redio cha Sudan CRN kuwa marais hao wawili watazungumzia mgogoro wa Abyei katika kutaka kuboresha uhusiano kati ya nchi hizo mbili.
Kuhusu swala la kura ya maoni kuhusu Abyei , waziri alisema kuwa Muungano wa Afrika hauruhusu uamuzi wa pande moja kuhusu kura ya maoni.
Aliongeza kuwa Kura ya maoni lazima iruhusiwe na nchi hizo mbili na kuidhinishwa na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.
Aidha alisema kuwa sudan Kusini inashurutishwa na makubaliano ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili na kwa hivyo haiwezi kuunga mkono kura ya maoni inayoshinikizwa na upande mmoja.
Hata hivyo alisema anaelewa kwa nini jamii ya Abyei iliamua kupiga kura ya maoni kujitenga na ni kwa sababu ya masaibu waliyoyapitia.
Alisisitiza kuwa Muungano wa Afrika na Sudan lazima ziisikilize jamii ya Abyei na kukubaliana kuhusu tarehe ya kufanyika kwa kura ya maoni kuhusu kutaka kujitawala wenyewe.
POSTED BY:www.info@dirayetu.blogspot.com
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment