UEFA CHAMPION LIGI; LEWANDOWSKI AIUA ARSENAL KWAO EMIRATES!!


CHELSEA YAPETA GERMANY, TORRES SHEREHE MECHI 100 NA BAO 2!!
SAN SIRO: AC MILAN, BARCA NGOMA NGUMU!!
LEWANDOWSKI-SHUJAA

UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, Usiku huu imeingia kwenye Mechi zake za Tatu kwa Makundi na Arsenal kubwagwa kwao Emirates kwa Bao 2-1 na Borussia Dortmund huku wenzao Chelsea wakiitwanga Schalke Bao 3-0 Nchini Germany na huko San Siro, AC Milan na Barcelona zilitoka Droo ya Bao 1-1.


ARSENAL 1 BORUSSIA DORTMUND 2
Robert Lewandowski alifunga Bao la Pili zikiwa zimesalia Dakika 8 Mpira kwisha baada kuunganisha Krosi ya Kevin Grosskreutz na kuipa Borussia Dortmund ushindi wa Bao 2-1 dhidi ya Arsenal Uwanjani Emirates.
Henrikh Mkhitaryan ndie alieifungia Dortmund Bao la Kwanza baada Aaron Ramsey kuupoteza Mpira karibu na boksi lakini Arsenal walisawazisha kwa Bao la Olivier Giroud kufuatia Krosi ya Bacary Sagna.

MAGOLI:
Arsenal 1
-Giroud Dakika ya 41 
Borussia Dortmund 2
-Mkhitaryan Dakika ya 16
-Lewandowski 82

LEWANDOWSKI-SHUJAAHata hivyo, Arsenal watahisi uonevu maana Lewandowski alionekana kuwa na bahati kubwa kubaki Uwanjani bila Kadi Nyekundu baada kumpiga kiwiko Sentahafu wa Arsenal Laurent Koscielny  mapema kwenye Kipindi cha Pili.
VIKOSI:
Arsenal: Szczesny, Sagna, Mertesacker, Koscielny, Gibbs, Ramsey, Arteta, Wilshere, Ozil, Rosicky, Giroud
Akiba: Fabianski, Vermaelen, Monreal, Cazorla, Bendtner, Jenkinson, Gnabry.
Borussia Dortmund: Weidenfeller, Grosskreutz, Subotic, Hummels, Schmelzer, Bender, Sahin, Blaszczykowski, Mkhitaryan, Reus, Lewandowski
Akiba: Langerak, Hofmann, Aubameyang, Kirch, Schieber, Papastathopoulos, Durm.
Refa: Jonas Eriksson (Sweden)
SCHALKE 0 CHELSEA 3
Fernando Torres amesherehekea kuanza Mechi yake ya 100 akiwa na Chelsea kwa kufunga Bao mbili huko Germany walipoichapa Schalke 3-0 na kutua kileleni mwa Kundi E.
Bao la Tatu la Chelsea lilifungwa na Eden Hazard.
VIKOSI:
Schalke: Hildebrand, Uchida, Howedes, Matip, Aogo, Jones, Neustadter, Clemens, Meyer, Draxler, Boateng
Akiba: Fahrmann, Hoogland, Felipe Santana, Kolasinac, Goretzka, Fuchs, Szalai.
Chelsea: Cech, Azpilicueta, Terry, Cahill, Ivanovic, Oscar, Ramires, Lampard, Schurrle, Torres, Hazard
Akiba: Schwarzer, Luiz, Mata, Mikel, Willian, Eto'o, Bertrand.
Refa: Viktor Kassai (Hungary)
AC MILAN 1 BARCELONA 1
Uwanjani San Siro, AC Milan na Barcelona zilitoka Sare ya Bao 1-1 huku Robinho akiifungia AC Milan katika Dakika ya 9 na Lionel Messi kusawazisha katika Dakika ya 24.
VIKOSI:
AC Milan: Amelia, Abate, Zapata, Mexes, Constant, Montolivo, De Jong, Muntari, Birsa, Robinho, Kaka.
Akiba: Coppola, Matri, Poli, Nocerino, Silvestre, Emanuelson, Balotelli.
Barcelona: Valdes, Dani Alves, Pique, Mascherano, Adriano, Iniesta, Busquets, Xavi, Alexis, Messi, Neymar.
Akiba: Pinto, Montoya, Fabregas, Pedro, Bartra, Song, Tello.
RATIBA-Mechi za Tatu:
Jumatano 23 Oct 2013
Bayer 04 Leverkusen v FC Shakhtar Donetsk
Manchester United FC v Real Sociedad de Fútbol
Real Madrid CF v Juventus
Galatasaray A.Ş. FC København
RSC Anderlecht v Paris Saint-Germain
SL Benfica v Olympiacos FC
PFC CSKA Moskva v Manchester City FC
FC Bayern München v FC Viktoria Plzeň
POSTED BY:www.info@dirayetu.blogspot.com
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment