Rais Jakaya Kikwete, amempongeza Meya wa Manispaa ya Moshi, Jaffar Michael kwa kile alichosema ni kusimamia vizuri na kutekeleza Ilani ya CCM katika kuwaletea wananchi maendeleo.
Kauli hiyo ya Rais Kikwete ambaye pia ni
Mwenyekiti wa taifa wa CCM ni nadra sana kutolewa na kiongozi wa CCM,
akipongeza utendaji mzuri wa viongozi wanaotoka vyama vya upinzani.
Meya huyo anatokana na chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), ambacho ndicho kinachoongoza Baraza la Madiwani kwa
kuwa na theluthi mbili ya madiwani wote wa Halmashauri.
Rais Kikwete alitoa pongezi hizo juzi wakati
akifungua jengo la kisasa la kibiashara lililojengwa katikati ya mji wa
Moshi na Shirika la Mfuko wa Hifadhi za Jamii (NSSF) kwa gharama ya Sh64
bilioni.
“Hata Mstahiki Meya nakupongeza kwa sababu nyinyi
hamna Serikali sisi (CCM) ndio wenye Serikali,”alisema Rais Kikwete
huku akicheka kwa furaha na kuongeza kusema;
“Kwa hiyo tunawashukuru kwa utekelezaji mzuri wa
ilani ya CCM na kwa sababu mnatekeleza vizuri, tutaendelea kuwapeni pesa
ya kuhudumia wananchi wa Tanzania,” alisema Rais Kikwete.
Rais Kikwete alitumia tukio hilo kuuagiza mkoa wa
Kilimanjaro, kutenga maeneo ya uwekezaji na kumtaka Meya huyo awe ni
Meya wa maendeleo kwa kutengeneza mazingira rafiki ya uwekezaji.
0 comments:
Post a Comment