CLUB YA WAANDISHI WA HABARI NA UTANGAZAJI ARUSHA WATEMBELEA VITUO VINNE VYA REDIO!!

Wanachama wa Club ya Waandishi wa Habari na utangazaji (AJTC) katika Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha wamefanya ziara yakutembelea vituo vipatavyo vinne Mkoani Arusha kwa lengo la kujifunza kinadharia na vitendo.

Ziara hiyo imefanyika kwa lengo la kuwafundisha wana Club namna ambavyo Redio zinaandaa matangazo, Habari,na Matukio mbalimbali hadi kumfikia Mskilizaji ikiwa ni moja ya masomo wanayosoma Chuoni hapo.


Pamoja na hayo Club ya JBC kwakutambua umuhimu wa elimu waliyokuwa wanakwenda kuipata ikiwa ni moja ya sera yao ya kujifunza kwa  nadharia na vitendo pia iliwashirikisha wanafunzi wa Chuo hicho wasiokuwa wanachama wa Club kwa lengo lakuonyesha mshikamano.

Miongoni mwa Redio walizotembelea ni pamoja na Redio Five iliyopo maeneo ya Njiro, Redio Safina,Triple A fm,pamoja na Mambo Jambo Fm.

Katika ziara hiyo wanachama hao walipata fursa yakuzungumza na watu tofauti tofauti wa Idara mbalimbali na kuuliza maswali ili kujijengea uelewa zaidi wa jinsi vipindi vinaandaliwa hadi kufika kwa msikilizaji.
Sanjari na hayo ikiwa ni kuangalia namna ambavyo mfumo mpya wa Sayansi na Tekinologia unavyofanyakazi.

Ziara hiyoiliongozwa na Waathiri mbalimbali wa Chuo hicho cha Uandishi wa Habari na Utangazaji akiwepo Bw.Elifuraha Samboto alimaarufu kama DJ,Christian Ndege,Onesmo Eliya Mbise pamoja na Lucas Modaha ambaye ni mlezi wa Club hiyo.

Pata Habari Picha;

Wanachama wa Club ya Uandishi wa Hbari na Utangazaji (JBC) katika Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji wakiwa nje ya magari  waliyosafiria mmara baada yakufika  Eneo la Njiro Arusha kilipo kituo cha REDIO FIVE.
Jengo la kituo cha kurushia Matangazo cha REDIO FIVE kwa nje.
;




Wanachama wa Club ya Uandishi wa Hbari na Utangazaji (JBC) katika Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji wakiwa nje ya magari  waliyosafiria mmara baada yakufika  Eneo la Njiro Arusha kilipo kituo cha REDIO FIVE.

Waathiri wa Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha kutoka kushoto kabisa Onesmo Eliya Mbise, Lucas Modaha pamoja na Christin Ndege Wakikaribishwa na mmoja wa wafanyakazi wa kituo cha Redio Five (Aliyesimama Mlangoni)katika kituo hicho.
Steshen Meneja wa kituo cha kurushia matangazo cha Redio Five (katikati) akitoa maelezo kwa wanaclub namna wanavyotakiwa kuona umuhimu wa kazi wanayosomea itakavyowasaidia pindi watakavyokuwa wamemaliza mafunzo yao.

Baathi ya wana Club wakiskiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Steshen Meneja.

Baathi ya wana Club pamoja na mwalimu wao kushoto wakiwa katika ukumbi wa mikutanoWakiskiliza kwa Makini umuhimu wakufanya vikao kwa wafanyakazi kila mara.
 

Wana Club wakikielezewa mikoa inakosikika  Redio Five kutoka kwa Mmoja wa Wafanyakazi wa kituo hicho.  
 
Watangazaji wa kituo cha Redio Five wakiwa na wana Club ya JBC ndani ya Studio wakiwapa maelekezo namna ambavyo mfumo wa vipindi unavyorushwa hewani

Mmoja wa mwanachama wa JBC Mwajuma Abduli akionyesha uwezo wake wakutangaza habari ndani ya studio za Redio five.

Mmoja wa mwanachama wa JBC Virginia Chidiaka akionyesha uwezo wake wakutangaza habari ndani ya studio za Redio five.
Wana Club wakiwa Chumba cha uandaaji wa matangazo na kurekodia sauti kwa vipindi mbalimbali.
Muathiri wa Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha Bw.Christian Ndege (kulia) akiwa na baadhi ya wafanyakazi wa kituo cha Redio Five nje ya jengo mara baada ya kutembelea Idara mbalimbali ndani ya kituo hicho.

Hili ni eneo linalotarajiwa kufanywa Stesheni ya televishen ikiwa ni moja ya malengo ya kituo hicho cha Redio five hapo baadae.
Mwalimu Elifuraha Samboto (mwenye Tshirt ya Njano)akitoa maelezo mafupi mara baada yakufika kituo cha Redio Safina.

Makamu wa Rais katika Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha akipita mbele kwenda kuangalia Utaratibu utakavyokuwa wakati wakutembelea Studio hizo za Redio Safina.



Wakiwa ndani ya kituo cha redio Safina Waadhiri wa Chuo cha Uandishi wa Habarina Utangazaji Arusha Bw.Chrisian Ndege (aliyekaa kulia) Elifuraha Samboto,Onesmo Elia Mbise walio simama nyuma pamoja na Mtangazaji wa kituo hicho Bi.Agnes Mayagila Samboto. 

Bi,Agnes Mayagila Elifuraha Samboto akitoa maelezo namna ambavyo shughuli za kuandaa na kurekodi vipindi unavyokuwa katika Redio Safina.


Muandaaji wa vipindi katika Stesheni ya Triple A fm akitoa maelekezo kwa Wana Club ya JBC.









Mara baada ya kuzunguka katika vituo hivyo vya redio nakujionea mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupata elimu jinsi uendeshwaji wa vituo vya Redio unavyokuwa wanafunzi hao walirejea Chuoni na kupata Mlo wa Jioni wakiwa pamoja na Waadhiri wao katika katika Kantini ya Club hiyo ya JBC ambayo pia ndiyo inayohudumia Waathiri wa Chuo, Wanafunzi pamoja na Wageni mbalimbali kutoka nje ya Chuo hicho na ndani ya Chuo.

Picha na Habari:Emanueli Onesmo Ndanshau.
POSTED BY:www.info@dirayetu.blogspot.com
















Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment