Rais wa UJERUMANI yupo nchini kwa ziara ya siku 5

Rais wa UJERUMANI, JOACHIM GAUCK na mwenyeji wake Rais JAKAYA KIKWETE
Rais wa UJERUMANI, JOACHIM GAUCK ambaye amewasili nchini jana na ameanza ziara yake ambapo amepokewa katika Viwanja vya Ikulu Jijini DSM na mamia ya wananchi wakiongozwa na Rais JAKAYA KIKWETE.

Mara baada ya kuwasili katika viwanja hivyo Rais JOACHIM GAUCK alipigiwa mizinga Ishirini na Moja ambapo baadaye nyimbo za taifa za TANZANIA na UJERUMANI zilipigwa.

Rais huyo wa UJERUMANI na mwenyeji wake Rais JAKAYA KIKWETE wamekagua graride rasmi la vikosi vya Jeshi la Wananchi wa TANZANIA - JWTZ ambapo viongozi hao wanakutana kwa mazungumzo ya faragha.

Kisha Rais KIKWETE akafanya mazungumzo maalum na mgeni wake na kisha kukutana na waandishi wa habari

Katika ziara yake Rais JOACHIM GAUCK ameambatana na ujumbe wa wafanyabiashara TISA wa UJERUMANI ambao wanataka kuwekeza hapa nchini ambapo baadaye kiongozi huyo atakutana na wafanyabiashara wa TANZANIA na wale wa UJERUMANI kuona namna wanavyoweza kushirikiana kibiashara.

Aidha rais GAUCK ambaye ataongozana na mkewe Bibi SCHADT, viongozi waandamizi na Ujumbe wa Wafanyabiashara kutoka nchini UJERUMANI , ataondoka DSM kwenda ZANZIBAR Februari NNE ambapo atafanya mazungumzo rasmi na rais wa Zanzibar Dkt. ALI MOHAMMED SHEIN kabla ya kushiriki kwenye Mkutano wa Kamati ya Pamoja ya Viongozi wa Dini kuhusu Amani.

Baadaye FEBRUARI 5, Rais huyo wa Ujenrumani atakwenda Mkoani ARUSHA ambapo atatembelea Taasisi mbalimbali za kimataifa ikiwemo Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, Jumuiya ya Afrika Mashariki –EAC- na atalihutubia Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki –EALA.

Rais GAUCK anatarajiwa kumaliza ziara yake hapa nchini tarehe 06 Februari, 2015 na kurejea nchini UJERUMANI.

Rais JOACHIM GAUCK yuko katika ziara hapa nchini kufuatia mwaliko wa Rais JAKAYA KIKWETE ambaye hivi karibuni alikuwa nchini UJERUMANI katika mkutano wa kimataifa wa kuchangisha fedha kwa ajili ya chanjo kwa watoto duniani.

Katika mkutano huo Rais KIKWETE ametunukiwa nishani kwa mchango wake katika kuhamasisha chanjo kwa watoto.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment