TWANGA PEPETA YAPANIA VALENTINE DAY LEO MANGO GARDEN!!


BENDI ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ usiku wa leo itafanya onyesho maalum ya kusherekea siku ya wapendanao ‘Valentine Day’, kwenye ukumbi wao wa nyunmbi Mango Garden Kinondoni.

Mkurugenzi wa bendi hiyo Asha Baraka amesema pia kuwa kupitia onyesho, hilo watatambulisha nyimbo zao mpya zilizoko kwenye chati.
Pia mkurugenzi huyo alisema kuwa bendi hiyo itapiga nyimbo zao zote za zamani zilizovuma wakati huo.

Aliwataka mashabiki wa bendi hiyo kujitokeza kwa wingi kuhudhuria onyesho la aina yake ambalo  litabubikwa na zawadi kibao za Valentine.

“Tumejianda vizuri kwa onyesho la Valentine. Onyesho hili limeboreshwa zaidi ya lile la kumpongeza mwanamuziki wao kongwe Lwiza Mbutu lililofanyika wiki iliyopita ambalo iliudhuriwa na umati wa mashabiki,” alisema Asha.

“Tunaomba watu wajitokeze kwa wingi waje waangalie onyesho letu  maalum  kwani ukizingatia kwamba Valentine Day hufanyika mara moja kwa mwaka,” alisema Asha.

Naye mratibu wa onyesho hilo Joseph Kapinga amesema kuwa maandalizi yote yamekamilika kilichobaki ni muda kufika ili mashabiki wapate uhondo.

Onyesho hilo limeandaliwa na Bob Entertainment na Keen Arts kwa hisani ya Dodoma Wine, Freditto Entertainment, CXC Africa
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment