MUHTASARI WA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2014; UFAULU WAPANDA KWA 10%!!




Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa Dkt Charles Msonde 


Jumla ya Watahiniwa 196,805 sawa na 68.33% ya watahiniwa wote waliofanya mtihani kidato cha IV mwaka 2014 wamefaulu ikiwa ni ongezeko la 10.08% kulinganisha na mwaka 2013 ambapo wanafunzi 235,227 sawa na 58.25 walifualu.
Akitangaza matokeo ya Kidato cha Nne ya mwaka 2014 leo jijini Dar es salaam, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa Dkt Charles Msonde amesema kati ya waliofaulu, wasichana ni 89,845 sawa na asilimia 66.61 wakati wavulana ni 106,960.
Amesema watahiniwa wa shule waliofaulu ni 167,643 sawa na asilimia 69.76 ya waliofanya mtihani, wasichana wakiwa 75,950 sawa na asilimia 68.70 na wavulana 91,693 sawa na asilimia 70.67.
Amesema mwaka 2013 watahiniwa 201,152 sawa na asilimia 57.09 ya watahiniwa wa shule walifaulu mtihani huo hivyo ufaulu kwa wanafunzi wa shule umepanda kwa asilimia 12.67 mwaka 2014 ikilinganishwa na mwaka 2013. 
Akizungumzia ubora wa ufaulu, Dkt Msonde amesema kuwa jumla ya watahiniwa waliopata ufaulu mzuri wa madaraja ya Distinction, Merit na Credit ni 73,832 sawa na asilimia 30.72 wakiwemo wasichana 27,991 sawa na asilimia 25.32 na wavulana ni 45,841 sawa na asilimia 35.33.
Watahiniwa waliopata daraja la PASS 93,811 sawa na asilimia 39.04 na waliofeli kwa kupata daraja la FAIL 72,667 sawa na asilimia 30.24.
Kuhusu ufaulu wa masomo, Dkt Msonde amesema kuwa ufaulu katika masomo ya msingi umepanda kwa kati ya asilimia 1.28 na 11.22 ikilinganishwa na mwaka 2013.
Ufaulu wa juu kabisa umekuwa katika somo la Kiswahili ambapo asilimia 69.66 ya watahiniwa wote wamefaulu na ufaulu chini kabisa ni wa somo la Basic Mathematics ambapo asilimia 19.58.
Amesema Baraza limefuta matokeo ya watahiniwa 184 baada ya kubainika kufanya udanganyifu, kati yao 128 ni watahiniwa wa kujitegemea na 56 ni watahiniwa wa shule.


 Akizitaja shule kumi bora kwa ufaulu, Dkt Msonde amesema shule hizo ni

1.Kaizirege mkoa wa Kagera
2.Mwanza Alliance mkoa wa Mwanza
3.Marian Boys mkoa wa Pwani
4.St. Francis Girls mkoa wa Mbeya
5.Abbey mkoa wa Mtwara
6.Feza Girls mkoa wa Dar es salaam
7.Bethel sabs Girls mkoa wa Iringa
8.Marian Girls mkoa wa Pwani
9.Feza Boys mkoa wa Dar es laam.
Shule 10 za mwisho ni:
1.Manolo mkoa wa Tanga
2.Chokocho mkoa wa Pemba
3.Kwalugulu mkoa wa Tanga
4.Relini mkoa wa Dar es salaam
5.Mashindei mkoa wa Tanga
6.Njelekela Islamic Seminary mkoa wa Kigoma
7.Vudee mkoa wa Kilimanjaro
8.Mnazi mkoa wa Tanga
9.Ruhembe mkoa wa Morogoro
10.Magoma mkoa wa Tanga.

 Dkt Msonde Pia ametaja watahiniwa 10 waliofanya vizuri kuwa ni:
1.Nyakaho Marungu kutoka Baobab Pwani
2.Elton Sadock Jacob kutoka Feza Boys Dar es salaam
3.Samwel M Adam kutoka Marian Boys Pwani
4.Fainess John Mwakisimba kutoka kutoka St Francis Girls Mbeya
5.Mugisha Reynold Lukambuzi kutoka Bendel Memorial Kilimanjaro
6.Paul W Jijimya kutoka Marian Boys Pwani
7.Angel Lundgreen Mcharo kutoka St Francis Girls Mbeya
8.Atuganile Cairo Jimmy kutoka Canossa
9.Jenifa Lundgreen Mcharo kutoka St Francis Girls Mbeya
10.Mahmoud Dadi Bakili kutoka Feza Boys

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment