Kila ifikapoTarehe 4 ya mwezi wa pili, inatukumbusha kwamba tunapaswa kupambana na ugonjwa wa saratani, ambao ni tatizo kubwa sana duniani kwa sasa. Mwaka huu, siku hii maalum imepangwa kufikia matokeo chanya juu ya vita dhidi ya saratani, kupitia kauli mbiu inayosisitiza kuwa ufumbuzi wakutokomeza saratani upo ndani ya uwezo wetu. Kampeni ya mwaka huu 2015, Siku ya Saratani Dunia inalenga katika kuchagua kudumisha maisha yenye afya, kutoa, upimaji kwa wakati, tiba kwa watu wote na kuongeza ubora wa maisha.
Kulingana na repoti ya Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI) ya January 2014. Takwimu zinaonesha, kuna wagonjwa mia moja (100) wapya katika kila idadi ya watu laki moja (100,000). Hii inamaanisha kuwa kila mwaka nchini Tanzania kuna wagonjwa 44,000 wapya wa saratani nchini, kulingana na hesabu ya sensa ya mwaka 2012 kwamba Tanzania ina takriban watu 44,900,000.
Kwa mujibu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, wanawake wapatao 7,515 kuugua saratani ya kizazi, nchini Tanzania kila mwaka na 6,009 wanawake wanakufa kutokana na ugonjwa huo. Saratani ya kizazi inawakilisha 55% hadi 65% ya kesi zote za saratani kwa wanawake na 35% na 40% ya kesi zote za saratani kwa ujumla. Saratani ya kizazi na saratani ya matiti huwapata sana wanawake. Saratani ya Kaposi sarcoma, ikifuatiwa na saratani ya umio, kichwa na shingo, huwapata sana wanaume. Pia kuna ushahidi kwamba saratani ya tezi dume inakuwa kwa kiasi kikubwa sana. Vifo pamoja na kesi hizi mpya za kansa zinahitaji kuzuiliwa.
Siku ya Saratani Duniani inasimama kama jukwaa pekee ambalo linahamasisha na kuongeza uelewa wa matokeo na athari zitokanazo na ugonjwa huu. Hivyo, kuna mengi ya kufanywa nchini Tanzania na watu binafsi, jamii na serikali, kwa kuunganisha na kuhamasisha ufumbuzi huu na kuchochea mabadiliko chanya.
Katika kuadhimisha siku hii, Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI) imeanzisha kampeni ya ufahamu juu ya kansa kutoka tarehe 2 hadi 5 Februari. Kwa mujibu wa mjumbe wa kamati ya kampeni ya saratani Dk Chuwa “kampeni itahusisha uchunguzi wa bure wa saratani kwa watu Februari 4, 2015 katika taasisi hiyo’’
Taasisi ya kimataifa mashuhuri kwa matibabu, Hospitali ya Apollo itakuwa mwenyeji wa warsha ya siku moja Alhamisi, Februari 5 juu ya Upasuaji kwa kutumia Roboti, upandikizaji wa uboho (BMT) na mambo mengine muhimu yahusianayo na ugonjwa wa saratani katika hosipitali ya kansa ya Apollo, Hyderabad. Ikifuatiwa na mkutano ujulikanao kama Apollo Cancer Conclave and Cancer CI 2015 (Mkutano wa Kimataifa juu ya kutibu saratani, Elimu na Utafiti juu ya kansa) kutoka tarehe 6 hadi 8 February mwaka 2015 mjini Hyderabad”. Kwa kawaida mkutano huu hufanyika kila baada ya miaka miwili. Kati ya wajumbe 1800-2000 kutoka India na nchi nyingine watashiriki.
Mkutano utakuwa chini ya mwamvuli wa Umoja wa Mataifa wa Kudhibiti Saratani, Union for International Cancer Control (UICC) na Umoja wa tiba ya kansa wa Ulaya, European Society for Medical Oncology(ESMO). Majadiliano juu ya maendeleo mbalimbali katika teknolojia katika tiba ya saratani, tiba ya mionzi kutoa mbinu na ushahidi juu ya tiba ya saratani kwa ujumla.
Hospitali ya Apollo inaongoza vita dhidi ya sarati katika njia nyingi kama vile mipango ya kudhibiti mapema, elimu, kujenga ufahamu, makambi Tiba na Tiba, teknolojia ya kisasa, wataalamu wakubwa, bodi ya uvimbe na huduma ya kina, ikiwa ni pamoja upasuaji na ushauri. Wagonjwa wengi kansa huhisi mwisho wa maisha yao umefika pindi wanapogundulika kuwa na ugonjwa huu. Habari njema ni kwamba kansa inatibika, na lazima walau kutibiwa na mbinu jumuishi, upasuaji, mionzi, ambazo zinapatikana katika Apollo Hospital.
Wakati tukiadhimisha siku hii maalum waathirika wa kansa kutoka Tanzania ambao walitibiwa katika Hospitali ya Apollo wametoa shukurani zao za dhati kwa hospitali ya Apollo kwa kuweza kuwatibu ugonjwa huo. Bi Dina Pauline Bina, alitembelea Hospitali ya Apollo kwa ajili ya matibabu ya kansa alitibiwa na kupona kabisa. Anasema kwamba “Ni vizuri kwamba mtu alifikiria uwepo wa hospitali kubwa kama hii, kwa kuwa inasaidia sio tu watu wa India lakini pia nchi nyingine za Afrika. Katika maeneo mengine ambapo hakuna aina hiyo ya hospitali watu wengi wanakufa si kwa sababu wanapaswa kufa kwa wakati huo, lakini kwa sababu hawana huduma za afya zinazoweza kukabiliana na hali zao’’.
Anaongeza kuwa, “Kila siku nyumbani na familia yangu tunamshukuru Mungu kuwa nilipewa nafasi ya pili katika maisha na hii iliwezekana kupitia hospitali ya Apollo” Mume wake pia ametoa maoni juu ya uzoefu mzuri walioupata wakiwa hospitali ya Apollo. Aliongeza, “Madaktari wako makini, wenye nia ya dhati, na wana ujuzi katika huduma mbalimbali za matibabu maalum. Huduma za wauguzi ni nzuri sana na vyumba vya hospitali vinawekwa katika hali ya usafi na usalama.”
Mgonjwa mwingine aliyepona ugonjwa wa kansa ya kansa ya damu, kutoka Tanzania Bi. Zuhura Shaban Luzilla, anatoa shukrani zake kwa Dr. Ranjan Kumar Mohapatra, Mtaalamu katika hospitali ya Apollo, na Bibi Gathi kwa ajili ya kutoa huduma nzuri na sasa amerejea kwenye afya yake ya kawaida.
Dk Emmanuel Kandusi, Mwenyekiti na mwanzilishi wa Kampeni ya 50 Plus nchini Tanzania aliyepona saratani ya tezi dume. Alikuwa akiteseka kutokana na ugonjwa huo kwa muda wa miaka kadhaa, baadaye alihamishiwa hospitali ya Apollo na kutokana na maendeleo na upatikanaji wa vifaa muhimu na wafanyakazi, yeye ulihudumiwa vizuri na kwa mafanikio. Sasa yeye ni kiongoza wa kampeni ya saratani ya tezi dume.
Pamoja na ukweli kwamba wengi wa Tanzania wamegundulika na saratani, imekuwa ikipuuziwa na watu binafsi, jamii na Serikali juu ya umuhimu wa kuangalia afya zao mara kwa mara kutokana na hofu kwamba hakuna tiba ya saratani. Ugonjwa huu upo ndani ya uwezo wetu, tunaweza kupambana nawo.
0 comments:
Post a Comment