Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, mkoani
Manyara, Anatory Choya, amesema kuwa aliwapigia magoti wananchi wa
Kijiji cha Hydom, ili kuonyesha unyenyekevu kwa wananchi hao aliodai
walionekana kujazwa maneno ya uchochezi na wanasiasa ili wavuruge amani
.
Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, mkoani Manyara, Anatory Choya akiwa
amewapigia wananchi magoti kwa maana ya kuonyesha unyenyekevu.
Alisema kutokana fujo zilizofanywa na baadhi ya wananchi hao katika
mkutano wa hadhara uliofanyika majuzi, kwa nafasi yake angeweza kuagiza
hata Jeshi la Polisi kuwadhibiti watu, lakini misingi ya dini yake
haimruhusu kumdhuru mtu zaidi ya kumwonyesha unyenyekevu.
Alisema hali hiyo ndiyo iliyomfanya kuamua kupiga magoti na kumshtakia Mungu.
“Mimi ni mkristo, unyenyekevu ndiyo nguzo pekee ya kuonyesha upendo na
kudumisha amani. Ningeweza kuagiza polisi wawadhibiti, lakini sioni
sababu kwa kuwa hiyo siyo misingi ya utawala. Ndiyo maana nikaona bora
nitumie njia nyingine ya kumshirikisha Mungu mbele yao,”alisema Choya na
kuongeza:
“Wanasiasa wamekuwa wakipandikiza chuki kwa wananchi kwa makusudi kwa
lengo la kuvuruga amani lakini kwa kumweka Mungu mbele nina imani
tutafanikiwa ili siku moja tusije tukaingia kwenye mkumbo wa Syria na
Misri”
Choya alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akizungumza na Mwananchi
Jumapili, siku chache baada ya kitendo chake cha kupiga magoti mbeye ya
wananchi kwenye mkutano wake wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha
Haydom.
Mkuu huyo wa wilaya alidaiwa pia kuwalaani baadhi ya wakazi wa Kijiji
cha Haydom kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kumdharau na kutofuata maagizo
yake, wakati yeye amewasaidia katika kutatua migogoro mbalimbali
waliyokuwa nayo.
Tukio hilo la kusikitisha lilijitokeza baada ya wananchi wa kijiji hicho
kupinga agizo la Choya, lililowataka kufanya uchaguzi wa kaimu
mwenyekiti wa kijiji hicho, kabla ya kufanya uchaguzi mdogo, ambapo
walipinga kwa kudai kuwa hakuna sheria hiyo.
Mmoja wa wananchi hao alilumbana na mkuu huyo wa wilaya mbapo Choya
alijibu; “Nami nitarudi kwetu." Naye Tikin akasema tena: “Unasema
utarudi kwenu Biharamulo wakati hawakutaki kwani ulifukuzwa ubunge?”
Maneno hayo yalionyesha kumkwaza Choya ambapo alipiga magoti huku
machozi yakimlenga na kumwomba Mungu afanye jambo kwa watu wa Haydom
kwani wanamdharau kabla ya kujitokeza wazee watatu wa Haydom na kumwomba
msamaha mkuu huyo wa wilaya.
Mwananchi
0 comments:
Post a Comment