Mkurugenzi wa Kiwanda cha kusindika
mazao yatokanayo na maziwa cha ASAS, Fuad Abri akizungumza na wanafunzi
na wananchi waliojitokeza kwenye maadhimisho ya siku ya unywaji wa
maziwa mashuleni yaliyofanyika kwenye uwanja wa Samora, Manispaa ya
Iringa.
ASILIMIA 52 ya watoto wnye umri wa chini ya miaka mitano mkoa wa Iringa wana utapiamlo mkali.
Akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya unywaji wa maziwa mashuleni kwenye uwanja wa Samora Manuispaa ya Iringa, Kaimu mkuu wa mkoa wa Iringa, Gelald Guninita alisema tatizo hilo linaufanya mkoa wa Iringa kushika nafasi ya tatu kitaifa ikiwa nyumba ya Lindi yenye 54% na Dodoma yenye 56%.
Guninita ambaye ni mkuu wa wilaya ya Kilolo alisema mkoa wa Iringa hautakiwa kuwa na tatizo la utapiamlo kutokana na uzalishaji wa maziwa na chakula kwa wingi.
Mkoa wa Iringa unazalisha jumla ya lita 18.4 kwa mwaka kutokana na ng'ombe wa kisasa 16,800 ambapo kila mmoja anazalisha lita tisa kwa siku.
Alisema licha ya uzalishaji huo wa maziwa na vyakula vingine bado Iringa kuna tatizo kubwa la utapiamlo mkali wa watoto chini ya miaka mitano, wanawake wajawazito, wawawake wenye umri wa kuzaa, wagonjwa, wazee na watoto.
Alisema maziwa yana faida kubwa kwa jamii ikiwemo kuboresha na kuimarisha meno na mifupa, ukuaji bora wa mtoto, kuongeza kinga ya mwili na kusaidia katika mtandao wa ufahamu mwilini.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha kusindika mazao yatokanayo na maziwa cha ASAS Iringa, Fuad Abri alisema wanaishauri serikali na wadau mbalimbali kuweka mkakati wa unywaji wa maziwa mashuleni ili kuongeza kiwango cha utumiaji maziwa nchini.
Katika maadhimisho hayo Kiwanda cha ASAS kilitoa msaada wa madawati yenye thamani ya sh2.2m kwa shule za msingi Mlangali, Hoho na Saint Dominic. Chanzo:
Hakimu Mwafongo
www.info@dira yetu.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment