MSIGWA AMPONGEZA RAIS KIKWETE KWA MKAKATI WAKE WA KUPAMBANA NA UJANGILI

E84A9602_187c7.png

MBUNGE wa jimbo la Iringa mjini kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo (chadema)amempongeza Rais Jakaya Kikwete kwa mkakati wake wa kunusuru vitendo vya ujangili katika hifadhi za Taifa.

Huku mbunge huyo akidai kuwa anawajua viongozi mbali mbali na watu maarufu ambao wanaendelea kuendesha vitendo vya ujangili katika hifadhi ya Ruaha Iringa ikiwa ni pamoja na kulitumia gari la wagonjwa (Ambulence) kusafirisha meno ya tembo na atawataja wahusika bungeni.

Msigwa ambae ni waziri kivuli wa wizara ya maliasili na utalii alitoa pongezi hizo leo mjini Iringa wakati wakati akifungua kikao cha kujadili vitendo vya ujangili katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha Iringa iliyoandaliwa na taasisi isiyo ya kiserikali ya Mazingira Netwark Tanzania (MANET).
"Awali ya yote napenda kumshukuru sana Rais Jakaya Kikwete kwa kuja na mikakati ya kweli ya kupambana na vitendo vya ujangili nchini kwa kutumia askari wa jeshi la lawanchi Tanzania (JWTZ)...huu ni mkakati mzuri ambao binafsi nimempongeza sana kwa hatua hiyo" alisema Msigwa
Kuwa ni mara kadhaa watanzania wamepata kusikia viongozi wa Serikali wenye dhamana wakisema kuwa mtandao wa majangili na wafanyabiashara haramu wa wanyamapori ni mpana na mgumu kuumaliza
Pia ni mara kadhaa pia Serikali imeendelea kukiri kuwa mtandao huu unawahusisha Wafanyabiashara wakubwa, Wanausalama, Wabunge, Wanasiasa na watu wenye dhamana ya uongozi katika taifa letu umekuwa ni kikwazo kikubwa katika vita dhidi ya ujangili.
"....Serikali imeendelea kutoa matamko kuwa itawataja wahusika wa biashara haramu dhidi ya wanyamapori na kuwachukulia hatua lakini cha kushangaza, mara zote hakuna hatua yoyote inayochukuliwa..ni jambo moja la msingi ambalo ningependa kulizungumza na kusisitiza hapa leo ni juu ya wajibu wa kila Mtanzania katika kuhakikisha kuwa tunaungana kwa pamoja katika vita dhidi ya biashara haramu ya wanyamapori"
Hivyo alisema hatua ya Rais Kikwete kuweka mkakati huo wa kutumia askari wa JWTZ katika kulinda hifadhi na kupambana na majangili ni jambo la kumpongeza.
Kwani alisema baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika tamko lake maarufu mwaka 1961 lijulikanalo kama Arusha Manifesto alisema yafuatayo
"Uhai wa wanyamapori ni jambo muhimu na linalotuhusu sana sisi sote barani Afrika. Viumbe hawa wa porini, wakiwa katika mapori wanamoishi,sio muhimu tu kwa ajili ya kuajabiwa na kuvutia lakini pia ni sehemu ya maliasili yetu na pia ndio mustakabali wa maisha yetu ya baadaye".
Alisema kuwa mwalimu Nyerere alitambua umuhimu wa kutunza wanyamapori kwa wakati huo tukiwa na hazina kubwa ya wanyama, lakini leo viongozi wa Serikali wameshikwa na kigugumizi katika kuhakikisha dira na jitihada za baba wa taifa letu ,vinatimizwa.
Hivyo alisema kama kiongozi ambaye wananchi wamenipa dhamana ya kuwawakilisha, nawiwa kutumia nafasi hiyo, kuendeleza juhudi zangu na kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa kila Mtanzania anakua mdau nambari moja wa kupinga biashara haramu ya wanyamapori kwani si tu kuwa inalitia hasara taifa letu bali pia inaweka hatarini maisha ya wanyamapori kwa vizazi vijavyo.
"Nachukua nafasi hii kuikumbusha na kuitaka Serikali kutimiza wajibu wake kwa kuwafikisha majangili na wafanyabiashara haramu wa wanyamapori katika vyombo vya dola na watendewe ipasavyo kwa mujibu wa Sheria"
Kuhusu watu maarufu mkoani Iringa wanaojihusisha na biashar a ya pembe za ndovu na hata kutumia magari ya umma kama Ambulence kusafirisha pembe hizo za ndovu alisema kuwa ana idadi yao ndevu zaidi na kuwa katika kikao cha bunge kijacho ataweka hadharani majina yao.
Kiongozi wa wanaharakati wa mtandao wa kupambana na vitendo vya ujangili katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha Fundi Mihayo alisema kuwa mbinu mbali mbali zinatumika katika kusafirisha pembe za ndovu ikiwa ni pamoja na usafiri wa boda boda kutumika sasa kuendeshea vitendo vya ujangili .
Alisema usafiri huo umekuwa ukitumika kuvushia pembe za ndovu katika maeneo ya vizuizi na hivyo kutaka ulinzi na upekuzi mkubwa unahitajika katika kukomesha vitendo hivyo.
Kwa upande wake mwenyekiti wa MANET Zuberi Mwachura alisema kuwa lengo la mtandao huo ni kuendelea kupambana na vitendo vya ujangili katika maeneo ya hifadhi nchini .
Kwani alisema kuwa usalama wa wanyama pori na mazingira yao ni walazima kwa maendeleo yetu hivyo ni wajibu wa kila mmoja wetu kujua na kufahamu eneo ambalo wanatoka au wanaishi watu wanao fanya au kushiriki au kujihusisha na vitendo vya ujangili ni jukumu letu kuhamasisha jamii ya wananchi wote wajione wana wajibu wa kushiliki katika vita dhidi ya ujangili.
"..lazima tukubali kwamba ujangili upo, Pamoja na changamoto zake, lakini hatuwezi kukaa kimya tukiacha majangili waendelee kuteketeza tembo wetu. .... Mwanzo wa mafanikio katika jambo lolote ni dhamila na nidhamu, ya kupanga na kutekeleza. ..... Kwa kukubaliana katika nia hii ya kupambana na ujangili ni vizuri tuwe na tamko la dhamira yetu ya kujinasua katika Lindi Kubwa la ujangili wa Tembo"

www.Info@Dira Yetu.blogspot.com 
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment