Vijana waliochaguliwa kujiunga na JKT
awamu ya tatu na pia waliochaguliwa kujiunga na vyuo vya elimu ya juu, ambao
wanataka kuahirisha mkataba wa JKT, wametakiwa kuandika barua Makao
Makuu ya JKT kuomba kuahirisha mkataba wa JKT.
Barua hizo wametakiwa kuambatanisha mambo yafuatayo ili kuweza kuhakikiwa ipasavyo kwakuhofia udanganyifu unaoweza kutumika.
Baadhi ya vitu walivyotakiwa kuambatanisha katika barua hizo ni pamoja na-
1.kuandika Barua binafsi ya kuomba kuahirisha mkataba pia ikiwa na kiambatanisho cha picha.
2. Nakala ya barua ya kuchaguliwa kujiunga na chuo husika(Joining instructions)
3. Barua hiyo ieleze kuwa utajiunga na JKT baada ya kuhitimu masomo.
4. Barua zote zifike Makao Makuu ya JKT kabla ya tarehe 02 Kotoba, 2013.
ANGALIZO
Kujiunga na JKT kwa mujibu wa sheria ni lazima. Hivyo ni wajibu wa kila mhitimu kuhudhuria mafunzo hayo.
Agizo hili limetolewa na Jeshi la Kujenga Taifa, Makao Makuu.
Source: http://www.wavuti.com/#ixzz2g4C18z5v
0 comments:
Post a Comment