NAIBU Spika wa Bunge la Tanzania
na Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai, katika Mkutano wa 12 wa kikao cha 2
cha Bunge Dodoma Jumatano, Agost 28, 2013, alishindwa kuvumilia na
kuficha hisia zake akataja mapungufu waliyonayo wapiga kura wake na
watanzania dhidi yake.
Ndugai
alitoa kauli hiyo kabla ya kumpongeza Spika wa Bunge la Tanzania na
Mbunge wa Njombe, Anne Semamba Makinda, ambaye hivi karibuni
alichaguliwa kuwa Rais wa Mabunge ya Afrika kwa Jumuia ya Madola.
Bila
kuuma maneno Ndugai alisema,”Watanzania wamekuwa na mapungufu ya
kutoenzi kazi nzuri zilizofanywa na viongozi na kuwapongeza walipofanya
vizuri, badala yake wamekuwa wakitanguliza Lawama za kuwalaumu, jambo
linalokatisha tamaa na kipunguza Moyo wa kujituma”.
Ndugai
alitolea mfano wa jimboni kwake ambako alisema, hakuna Mradi wowote kwa
mfano Ujenzi wa Choo, Zahanati, Shule na Maendeleo mbalimbali
yanyofanywa bila Mchango wake kuhusika, lakini hata siku moja hakuna
Mradi wowote ambao aliofanywa mgeni rasmi na kuufungua.
Nimekuwa
nikitoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya Jimbo langu, hakuna
kinachofanywa ambacho sihusiki kuchangia, lakini ikifika wakati wa
ufunguzi, wanafungua wengine hivyo hadi nitakapomaliza kipindi change
sina kumbukumbu yoyote”.alisema Ndugai.
Alichosema
Ndugai ni ukweli usiopingika, kwani hivi karibuni nilifanya Ziara kati
shule moja ya Msingi ya NDC-NARCO Kongwa, ambayo baadhi ya Wabunge
katika Bunge lililopita walijitolea kuichangia ili kumalizia Jengo la
Kulala, lakini Viongozi wa Elimu (W) walisita kumwalika na badala yake
walitaka kumualika Mbunge mwingine.
Mmoja
wa viongozi hao wa Wilaya ya Kongwa alifikia mahali pa kumtishia
Mwalimu mmoja Jina linahifadhiwa, asijihusishe na Wanasiasa katika
kufanikisha Ujenzi huo na badala ya anamtaka afundishe, la sivyo
akifanya Mchezo atamhamisha.
Hoja
yangu ni kwamba, ni kwa nini Kiongozi mkubwa namna hiyo tena Naibu
Spika Bunge (Ndugai) hata Jengo au Barabara jimboni kwake lisiitwe kwa
Jina lake? Swala hili ndilo linamsibu Ndugai hata akatafuta mahali pa
kufikisha Ujumbe kwa wananchi wake na watanzania.
Pamoja
na kwamba kuna usemi usemao ajikwazaye atashushwa na ajishushaye
atakwezwa, tujiu;ize; Je. Kwa nini wananchi wa Jimbo la Kongwa, Viongozi
wa Mkoa wa Dodoma na Tanzania hawammpi fursa anayojipigia debe Mbunge
huyo hadi aipigie chapuo akipongezwa Makinda?
Wananchi na viongozi jimboni humo waliohojiwa kwa nyakati tofauti na kuombwa wasitajwe majina yao walidai,
“Ni
kweli sisi kama viongozi wa Elimu wilayani humu, tumekuwa tukimuita
Mbunge wetu mara kadhaa kwa ajili ya kuchangia shughuli mbalimbali za
Elimu, lakini amekuwa si mtoaji na mshiriki wa karibu wa shughuli
husika”.alisema mdau mmoja wa elimu wasioiva wilayani humo.
Mkulima
mmoja wa Mahindi na Alizetiwengi miongoni mwa wenzake wa Kijiji cha
Pandambili wilayani Mlali alimtuhu kama alivyowahi kumshitaki Meya wa
Musoma Alex Kasurura (Chadema) katika moja ya Mikutano jimboni humo
kwamba, Ndugai ameshindwa kuwatafutia Masoko ya mazao hayo wananchi wake
ingawa anajisifu kwa safari za kwenda nje kila mara.
Aidha
katika Malalamiko ya Ndugai dhidi ya Wapiga kura wake na Watanzania
kuwa hawampi nafasi au Fursa za kumuenzi hata kwa kumpa kumbukumbu za
Majina ya Miradi ya Barabara au Majengo ni kutokana na kutokuwa na
ushirikiano wa karibu na watu wake.
0 comments:
Post a Comment