Baada
ya kuwepo kwa fununu za uingizwaji wa samaki hao wanaodaiwa kuharibika kutoka
nje ya nchi kuingia hapa nchini na kuhatarisha maisha ya walaji,Itv
iliendelea kufuatilia tetesi hizo kwa kushirikiana na maafisa wa mamlaka
ya chakula na dawa nchini-Tfda kwa lengo la kuwabaini wahusika wa samaki
hao ambapo kwa eneo la tabata bima jijini dar es salaam kontena mbili
zilikutwa zikitumika kuhifadhia samaki wa aina tofauti ambapo katika
kontena ya kwanza inayomilikwa na kampuni ya SAIS Boutique inadaiwa
iliingiza samaki aina ya vibua tani 22.5 kutoa china julai 2013 na kwa
bahati mbaya samaki hao wamedaiwa kuharibika licha ya kuwa zilishaanza
kuuzwa sokoni tangu zilipofika.
Afisa
uhusiano wa mamlaka ya chakula na dawa nchini -Tfda Bi Gaudencia
Simwanza,ameeleza kusikitishwa kwa uwepo wa samaki hao waliharibika
katika kontena hiyo huku akiongeza kuwa kontena nyingine mali ya kampuni
ya Amasa Fish Traders iliyokuwa na samaki tani 27 aina ya vibua na
kolekole kutoka nchini Yemen lazima ichunguzwe pia ili kubaini usalama
wa samaki hao.
Mmiliki
wa kontena iliyokutwa na samaki zilizoharibika Bwana Sadick
Maporo,alikiri samaki wake kuharibika lakini akadai kuwa samaki hao
waliharibika baada ya kufika hapa nchini kutokana na kukatikakatika kwa
umeme.
chanzo ITV TANZANIA
0 comments:
Post a Comment