KUFUATIA KUSIMAMISHWA KWA UONGOZI WA MWENYEKITI WA CHADEMA MKOA WA ARUSHA; MJADALA MZITO WAZUKA, HAYA NDIYO YALIYOMFANYA MWENYEKITI ASIMAMISHWE.


- Baadhi ya wanachama wadai hoja zake zilikuwa na mashiko na haikutakiwa asimamishwe bali hoja ziangaliwe
- Wengine wadai hakutakiwa 'kuyaweka kwenye mitandao' angeyapeleka kwenye uongozi wa juu wa chama

Hiki ndicho alichoandika Mwigamba akiwashauri wanaCHADEMA kupitia=> 
http://bit.ly/1gxED3R
Fuatilia hapa alichokisambaza kwenye mitandao ya kijamii.


 Wito kwa wana CHADEMA wote!

Kufuatia malumbano yanayoendelea kwenye vyombo vya habari na madhaifu mengi ambayo tumeshayashuhudia kwenye chama kwa sasa, natoa wito kwa wana CHADEMA wote nchini kwamba wakati umefika tubadilishe uongozi wa juu wa chama.

Kihistoria, CHADEMA kati ya mwaka 2005 na 2010, agenda zetu kwa wananchi zilikuwa mbili. Kupiga vita ufisadi, iliyosukumwa sana na Dr. Slaa na ile ya utetezi wa raslimali zetu iliyobebwa na Zitto. Lakini sasa hivi chama kinaenda kwa matukio.

Naandika nikiwa mwana CHADEMA safi na nataka kila mwanachama atakayesoma atulie na kutafakari. Hili siyo jambo la ushabiki. Ni mawasiliano baina yetu wana CHADEMA na tunahitaji tutulie na kutafakari. 


Nimekuwa mwanachama wa siku nyingi na nimebahatika pia kuwa kiongozi ndani ya chama kwa nyakati tofauti kwahiyo naelewa ninachokiandika. Nadriki kusema kwamba kwa sasa chama kinakwenda kwa matukio na ni bahati tu kwamba CCM inaendelea kutupatia matukio lakini CCM na serikali yake wakitunyima matukio, CHADEMA chini ya Mkt Mbowe, Katibu mkuu Slaa na Naibu Zitto utakuwa ndo mwisho wake.

CHADEMA iliyopiga kelele sana dhidi ya ufisadi, CHADEMA iliyopiga kelele mpaka sheria ya vyama vya siasa ikabadilishwa na vyama kutakiwa kukaguliwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), eti leo inaungana na CCM kumshambulia mwenyekiti wa kamati ya bunge ya hesabu za serikali (PAC) kwa kutamka kwamba vyama havijawasilisha ripoti zake za fedha zilizokaguliwa. Kwa nini? Muungano huu wa CHADEMA na CCM maana yake nini? Kama chama kinajiamini ni kisafi kwenye hesabu zake hofu ni ya nini? Si wasubiri kikao na kamati ya bunge katibu mkuu aende na hizo ripoti na nyaraka zinazoonyesha kweli wamewasilisha hesabu hizo?

Napenda kabla sijaendelea mbele kuwapongeza wenyeviti wetu wawili wa kwanza ambao kimsingi waliweka msingi mzuri sana wakutong’ang’ania madaraka na badala yake kuachia mapema na kumwachia mwinginekidemokrasia bila vurugu. Hawakuwa madikteta na nawapongeza sana. Walijitahidi sana kutokuwa wapenda madaraka na kimsingi walituwekea utamaduni ambao walitaka wote tuufuate na kujenga taasisi imara inayojali demokrasia na haki ya kilamwanachama.

Ni kwa msingi huo waliamua kuandika kabisa katika katiba yetu kwamba kiongozi yeyote katika ngazi yoyote ya kuchaguliwa atakapogombea na kushinda ataongoza kwa kipindi kimoja cha miaka mitano na kisha ataweza kugombea nakuongoza kwa kipindi cha pili cha miaka mitano baada yapo hawezi kugombea tena katika nafasi ile ile aliyoitumikia kwa vipindi viwili. Ili kuonyesha kwamba walimaanisha kile walichokisema, wote wawili hawakuwahi kukaa madarakani kwa vipindi viwili vilivyoruhusiwa katika katiba bali wote wawili walikaa kipindi kimoja kimoja tu.


Napenda pia kumpongeza mwenyekiti aliyepo madarakani, Mbowe. Kuna mengi kakifanyia chama. Kakitoa kutoka kwenye chama cha tatu ama nne kwa upinzani hadi kuwa cha kwanza na kustahili kuitwa chama kikuu cha upinzani. Kakichukua kikiwa na wabunge 5 bungeni na leo katika kipindi chake cha miaka 10 kina wabunge 49. Ni achievement kubwa! Si hivyo tu, ni wakati wake CHADEMA imebeba agenda nzitoza kitaifa kama vile vita dhidi ya ufisadi, utetezi wa raslimali, katiba mpya,nk. 

Lakini kuna matatizo yameanza kujitokeza na tusipochukua hatua haraka huko mbele tunaweza kupata shida kubwa. Ni muhimu kwa Mbowe kuelewa kwamba uwezo wake umefikia hapo asitake kulazimisha kusonga mbele akidhani bila yeye hakuna CHADEMA. Akiache chama kikiwa salama, abaki kama mwenyekiti mstaafu na awaachie wengine awamu inayofuata ya kuingia madarakani. Kama hataki kuwa mwelewa na kuachia ngazi, wanachama tumsaidie kwa kumpiga chini uchaguzi ujao. Leo nitaainisha mambo machachetu yanayohusiana na fedha za chama na uaminifu ili wanachadema muelewe kwa nini viongozi wakuu wa chama wamehamaki sana kusikia wanatakiwa kuwasilisha ripotiza fedha wakajikuta wanapambana na mwenyekiti wa kamati ya bunge badala ya kamati na hata kufikia kusahau kwamba huyo mwenyekiti wa kamati ya bunge ni mwenzao, ni naibu katibu mkuu wa chama. Mengine nitaendelea kuyadondoa siku nyingine nitakapopata fursa:

1. Wakati tukifanya mabadiliko ya katiba mwaka 2006 hatukugusa kipengele kinachomzuia kiongozi kuongoza kwenye nafasi moja kwa zaidi ya vipindi viwili vya miaka mitanomitano. Lakini wakati katiba inachapwa chini ya uongozi uliopo, kipengele hicho kiliondolewa kinyemela. Mambo yanayotokea hivi leo yanaonyesha dhahiri kipengele hicho kiliondolewa kwa makusudi kwa maslahi na kwa faida ya viongozi waliopo madarakani kwa sasa. Hiki kinaweza kuchukuliwa kama kitendo kidogo lakini kama viongozi wetu wanaweza kutokuwa waaminifu katika jambo kama hili, ni dhahiri hawawezi kuaminika na wanaweza kufanya mambo mengine makubwa nayenye athari zisizomithirika kwa chama.

Ni muhimu wanachadema mkafahamu kwamba kitendo cha kuondolewa kwa kipengele hicho ndicho kinacholeta mpasuko leo kwenye chama unaotokana na Mbowe na Zitto kupigania uenyekiti. Kama kingekuwepoleo Mbowe alikuwa anakatazwa na katiba kugombea kipindi cha tatu na hivyo vita iliyopo kati yake na Zitto isingekuwepo na chama kingekuwa imara zaidi. Ni dhahiri Mbowe aliondoa kipengele hicho kwa makusudi ili aweze kuendelea kugombea bila mwisho na huu ni udikteta kama ule tu wa akina Lyatonga Mrema, John Cheyo na wengineo, na wanachadema hatupaswi kuuruhusu si kwa Mbowe tu bali kwa yeyote atakayepata nafasi ya kuwa mwenyekiti wa chama chetu.

2. Matumizi ya fedha za chama:
Hakuna mtu anayejua hivi sasa fedha za chama zinatumikaje zaidi yakakikundi ka watu watatu yaani Mwenyekiti Taifa, Katibu Mkuu na Mkurugenzi wa Fedha. Maamuzi ya vikao hayaheshimiki tena na mabwana hawa. Baada ya uchaguzi wa 2010 vikao halali vilielekeza kiasi na aina ya fedha ambazo hazitaguswa bali zitunzwe kwenye akaunti maalum kwa ajili ya uchaguzi wa 2015. Lakini leo si tu akaunti hiyo haina fedha bali hakuna akaunti yoyote yenye fedha. Watu watatu ndo wanaamua fedha zitumikeje. Mfano mwingine ni maamuzi ya kikao cha Baraza kuu cha mwezi January kilichoamua kwambakiasi cha fedha inayotoka serikalini kipelekwe kwenye mikoa, wilaya namajimbo na kiasi kingine kipelekwe kwenye kanda. Leo ni mwezi wa 10 maamuzi hayo hayajatekelezwa ipasavyo.

Nyinyi viongozi wa kanda,mikoa, wilaya na majimbo ni mashahidi wa hili . Lakini kuna michangoya watu binafsi kama Mzee Sabodo, hizo nazo hazijulikani zimechukuliwa lini kwa mfumo gani, zikatunzwa wapi na hatimaye zimetumikaje. Hapo sijataja fedha zinazopatikana kutoka kwenye fundraising events mbalimbali kama ile ya Dar es Salaam na Mwanza. Hizo nazo hazijawahi kuonekana na walioendesha hizo fundraising, uaminifu wao kwenye masuala ya fedha ni
questionable.

3. Taarifa za fedha
Tokea baada ya uchaguzi wa 2010 mpaka leo, hakuna kikao chochote kilichowahi kupokea na kujadili hadi mwisho ripoti ya mapato na matumizi ya fedha za chama. Kila kikao agenda hiyo inarushwa kiaina. Wanaojua mchezo huo ni watu watatu tuniliowataja hapo juu na malengo ya kurusha hiyo agenda kila wakati na kukwepesha isijadiliwe pia wanayajua wao. Ni dhahiri tukiendelea na hawa watu tutafika 2015 tukiwa hatuna pesa hata ya kuweka mawakala kwenye vituo na tutapigwa tukiwa tumesimama.

4. Mipango ya kukipatia chama mapato ya ziada kutoka nje ya chama
Wakuu waliopo hawana hata ndoto ya namna ya kupata fedha za ziada. Wanachokijua ni kukusanya ‘sadaka’ kwenye mikutano ya hadhara na kuwapatia kazi watu wanaoonekana kuwa matapeli eti waendeshe harambee za kuchangisha fedha kwa njia ya matukio. Mawazo mazuri kama la kuanzisha kampuni la uwekezaji la chama litakalowekeza kwenye miradi mbalimbali, halijawahi kufanyiwa kazi, nahivyo uanzishaji wa miradi mbalimbali ya kuiingizia taasisi fedha imebaki ndotoya mchana. Hatuwezi kufika hata siku moja bila fedha. Hata uchaguzi wa wenzetu wa Kenya juzi juzi wakuu wetu ingawa walishiriki lakini hawaonekani kama wamejifunza chochote.

5. Matumizi mabaya ya madaraka yanayoweza kuhusishwa na ufisadi
Chama chetu kinayo kamati ya tenda ambayo iko chini ya sekretariat. Lakini kamati hii haifanyi kazi imezimwa kimya kimya na wajumbe wote wa kamati ya tenda kwa kuwa ni wachumia tumbo wanaojigonga kwa wakuu,wamekubali kuzimwa. Leo ikidaiwa kamati hiyo ilete nyaraka za mchakato wa manunuzi ya magari, pikipiki, kadi za uanachama, set ya televisheni iliyofungwa ofisini kwa katibu mkuu, hawana. Manunuzi haya yote yanafanywa na wakuu bila utaratibu wowote jambo ambalo ni hatari na linarahisisha matendo ya kifisadi. Hivi tunavyoongea, ni mwenyekiti taifa mwenyewe ndiye aliyenunua magari napikipiki zote za M4C.

Hivi tunavyoongea kuna shilingi milioni 80 ambazo Mwenyekiti Taifa alizichukua na kuagiza kadi za uanachama tangu mwaka jana mpaka leo hizo kadi hazijawahi kuonekana. Na mwenyekiti anafanya mambo hayo yote akitambua kwamba yeye ni mwenyekiti na hayo ni masuala ya kiutendaji ambayo yako chini ya katibu mkuu kama mtendaji mkuu wa chama na kamati yake yatenda. Huu si ufisadi ni nini?

6. Makubaliano ya kifisadi na mtu binafsi anayeuza vifaa vya uenezi vya chama
Hakuna kikao chochote cha juu kilichojadili ama kilichowahi hata kupewa taarifa tu kwamba sasa kuna mtu binafsi kapewa tenda ya kuuza vifaa vya chama na chama kinanufaika vipi namauzo hayo na kwa nini vifaa muhimu vya chama kama bendera vinauzwa na mtu binafsi. Jambo hili linajulikana kwa Mwenyekiti Taifa na Katibu Mkuu wake tu.

Napenda kwanza kuipongeza kamati ya bunge kwa kuvikomalia vyama vinavyopokea ruzuku bila kujali ni chama tawala ama upinzani.

Pili namshauri CAG unaweza kutumia kampuni binafsi kwenye wizara, idara, taasisi, wakala, na asasi zote za kiserikali na serikali za mitaa kwenye ukaguzi lakini kamwe usiruhusu vyama vya siasa vikaguliwe na kampuni hizo. Hapo nenda mwenyewe ndo utajionea mwenyewe. Kampuni binafsi kwenye vyama huko zinafundishwa ziandikeje maoni yao. Nenda mwenyewe ujionee. 


Pia kuna mkakati unaendeshwa na CHADEMA Makao Makuu kwa sasa wa kuwapigia simu viongozi wa mikoa hasa hapa Dar es Salaam na mikoa mikubwa kama Mwanza, Arusha, Mbeya, nk, wakiwataka viongozi wa mikoani mtoe matamko kumpinga Zitto. Kataeni ushenzi huu. Hili si jambo la Zitto ni la kamati ya bunge na kimsingi ni la uadilifu ndani ya serikali na vyama. Hata kama jambo lenyewe lingekuwa limeagizwa na Mwigulu Nchemba msingetoa matamko ya kupinga zaidi ya kuwaacha viongozi wetuwakuu watoe ripoti kuthibitisha uadilifu wao japo kidogo maana ni ukweli piakwamba kwenye ripoti wanaweza kuzuga zikawa safi lakini ufisadi umefanyika. Kama ni matamko toeni matamko ya kuutaka uongozi wetu utoe hizo ripoti, na hapondipo mtakapojua kwanini hampati ruzuku. Kuna matumizi mengi sana ya hovyo na ufisadi mkubwa unafanyika hapo Makao Makuu.

Nitaendelea kuwadondolea ili muonekwa nini napendekeza tuung'oe uongozi huu chini ya Mbowe.

Ahsanteni kwakunisoma
!
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment