JUMANNE ya leo,
Februari 24,katika Uwanja wa Etihad Jijini Manchester utalipuka kwa mpambano
mkali wa Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA
CHAMPIONZ LIGI kati ya Manchester City na FC Barcelona.
Mechi hii ni
Marudio ya Mechi ya Msimu uliopita ya Raundi hii hii ya Mashindano haya
wakati Man City ilipotolewa na Barcelona kwa Jumla ya Mabao 4-1 katika
Mechi mbili ambazo kila Mechi City ilimaliza Mtu 10 baada ya Mchezaji
wao mmoja kupewa Kadi Nyekundu.
Katika Mechi hizo, Barcelona walishinda Mechi ya Kwanza iliyochezwa Etihad Bao 2-0 na
kwenye Marudiano huko Nou Camp, Barca ilishinda Bao 2-1.
Hali za Timu
Man City
itamkosa Kiungo wao mahiri Yaya Toure ambae anamalizia Kifungo chake cha
Mechi 3 alichopewa na UEFA lakini Straika wao mpya Wilfried Bony ruksa
kuanza Mechi hii.
Barcelona
huenda wakamchezesha Straika wao Luis Suarez ambae atakuwa akicheza
Mechi yake ya kwanza Nchini England tangu aihame Liverpool mwanzoni mwa
Msimu.
Tathmini
Man City
walishindwa kuvuka hatua ya Makundi ya UEFA CHAMPIONZ LIGI katika Misimu
ya 2011/12 na 2012/13 lakini katika Misimu miwili iliyopita walivuka na
kukwamia hatua ya Raundi hii.
Wiki
iliyopita, Timu zote zilikuwa kwenye Ligi za kwao kwa Barcelona kuchapwa
kwao Nou Camp Bao 1-0 na Malaga katika La Liga baada ya kushinda Mechi
11 mfululizo wakati City ikiitwanga Newcastle United Bao 5-0 kwenye Ligi
Kuu England.Timu zote hizo mbili zinashika Nafasi za Pili za Ligi za Nchi zao.
Akiongelea
mtanange huu wa Uwanja wa Etihad, Sentahafu wa Barca, Gerard Pique,
ambae aliichezea Man United ambao ni Mahasimu wakuwa wa City, alisema:
“Hii ni moja ya Gemu ya Mwaka, na ni muhimu kwetu kwa sasa. Watajaribu
kutushambulia na hilo linatufaa sisi. Imedhihirishwa kwamba tunakuwa
vyema dhidi ya Timu zinazotushambulia kwa sababu tunaweza kupiga kaunta
ataki!”
Nae Straika wa Man City, Sergio Aguero, ametamka: “Hii ni Gemu mpya na sisi sasa si sawa na Msimu uliopita na wao pia sivyo!”
Meneja wa City Manuel Pellegrini ameahidi Timu yake itacheza kwa kushambulia tu.
VIKOSI:
Manchester City: Hart, Clichy, Mangala, Kompany, Zabaleta, Fernando, Fernandinho, Nasri, Silva, Navas, Aguero.
Barcelona: Ter Stegen, Alves, Pique, Mascherano, Alba, Rakitic, Busquets, Iniesta, Neymar, Messi, Suarez.
REFA: Felix Brych (Germany)
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment