PAMBANO LA RUVU, SIMBA LAINGIZA MIL 75/-


UWANJA_WA_TAIFA_DAR
Pambano la Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya wenyeji Ruvu Shooting na Simba lililochezwa jana (Oktoba 5 mwaka huu) katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 75,692,000.

 Ripoti ya afisa  wa habari wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania{TFF} bwana Boniface Wambura ameeleza kuwa Watazamaji waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo namba 43 la VPL msimu wa 2013/2014 lililomalizika kwa timu hizo kutoka sare ya bao 1-1 walikuwa 13,395.

Viingilio katika mechi hiyo vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 17,983,902.31 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 11,546,237.29.

Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 9,144,357.11, tiketi sh. 3,183,382, gharama za mechi sh. 5,486,614.26, Kamati ya Ligi sh. 5,486,614.26, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,743,307.13, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA) sh. 1,066,841.66 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,066,841.66.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment