Ujerumani yakabidhi kambi ya Kunduz,Afghanistan.

Baada ya kipindi cha miaka kumi jeshi la Ujerumani Bundeswehr Jumapili(06.10.2013) limekamilisha jukumu lake kaskazini mwa Afghanistan kwa kukabidhi rasmi mamlaka ya kambi yao ya Kunduz kwa vikosi vya Afghanistan.

Mawaziri wa Ujerumani na Afghanistan wakishuhudia wakati maafisa waandamizi wa kijeshi wa Ujerumani na Afghanistan wakisaini nyaraka za makabidhiano ya kambi ya Kunduz. Mawaziri wa Ujerumani na Afghanistan wakishuhudia wakati maafisa waandamizi wa kijeshi wa Ujerumani na Afghanistan wakisaini nyaraka za makabidhiano ya kambi ya Kunduz.

Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Thomas de Maiziere na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Guido Westerwelle kwa pamoja wameikabidhi kambi hiyo kwa vikosi vya usalama vya Afghanistan katika ziara isiotangazwa iliofanyika Jumapili wakitokea kwenye kambi ya jeshi la Ujerumani ya Mazar-i-Sharif. Akizungumza katika hafla hiyo de Maiziere amezungumzia juu ya kujitolea roho zao kwa wanajeshi wa Ujerumani huko Kunduz ambapo 18 wameuwawa kutokana na mashambulizi na katika mapambano wakati wa kutimiza majukumu ya Kikosi cha Kimataifa cha Usaidizi (ISAF) chini ya usimamizi wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO.Amesema "Kwetu sisi Kunduz ni mahala ambapo Bundeswehr ilipigana kwa mara ya kwanza na ilibidi kujifunza kupigana.Huo ulikuwa wakati muhimu wa maamuzi sio tu kwa jeshi la Ujerumani bali pia kwa jamii ya Ujerumani."
Waziri huyo amesema juu ya kwamba jeshi la Ujerumani linaondoka katika jimbo hilo amesisitiza kwamba katu hawatolisahao kwa kuwa lina umuhimu mkubwa wa kiishara kwa jeshi la Ujerumani. Amesema Kunduz ni mahala ambapo imelishughulisha jeshi la Ujerumani kuliko mahala popote pale,hapo walijenga na kupigana,walilia na kujifariji,waliuwa na kuuliwa. de Maiziere amesema "Kunduz daima itakuwa sehemu ya kumbukumbu yetu ya pamoja."
@DW
POSTED  BY:www.info@dirayetu.blogspot.com
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment