YANGA WALIMWAGA, WAONGOZA 3-0 SIMBA YAPATA SARE 3-3!!

MABINGWA wa Tanzania Bara, Yanga, itabidi wajilaumu sana maana walishawaweka Simba DABI_YA_KARIAKOOpabaya sana kwa kumudu kuongoza Bao 3-0 hadi kipindi cha kwanza kuisha leo hii Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam lakini Simba waliibuka Kipindi cha Pili na kusawazisha Bao zote na Mechi hii ya VPL, Ligi Kuu Vodacom kumalizika kwa Sare ya Bao 3-3.

MAGOLI:
Simba 3
- Betram Mombeki Dakika ya 54
-Joseph Owino 58
- Kaze Gilbert 85
Yanga 3
-Mrisho Ngassa Dakika ya 15
-Hamis Kiiza 36
-Hamisi Kiiza 45

Ni wazi uamuzi wa Kocha wa Simba Abdallah Kibaden kubadilisha Kikosi chake na kuwaingiza Said Ndemla na William Lucian badala ya Haruna Chanongo na Abdulhalim Humud mwanzoni mwa Kipindi cha Pili kuliwasaidia Simba kupata Sare hii.
VIKOSI:
Simba: Abbel Dhaira, Nassor Masoud ‘Chollo’, Haruna Shamte, Gilbert Kaze, Joseph Owino, Jonas Mkude, Haruna Chanongo [Said Ndemla], Abdulhalim Humud [William Lucian], Betram Mombeki [Zahor Pazi], Amisi Tambwe, Ramadhani Singano.

Yanga: Ally Mustafa ‘Barthez’, Mbuyu Twite, David Luhende, Nadir Haroub, Kevin Yondan, Athumani Iddi ‘Chuji’, Mrisho Ngassa, Frank Domayo, Didier Kavumbangu, Hamisi Kiiza [Simon Msuva], Niyonzima.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment