WANASHERIA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI KENYA,RWANDA NA UGANDA WAFULIWA KESI!!

Wakili Jimmy obedi akiwa anakabidhi nyaraka za kesi dhidi ya serikali za
Kenya,Rwanda na Uganda,kwa Afisa masijala wa mahakama ya Afrika ya
mashariki Boniface Ogoti jana.kulia ni mmoja wa walalamikaji Ally msangi.
 Wanasheria wakuu wa nchi  za Kenya,Rwanda na Uganda wamefunguliwa
mashitaka katika Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kutokana na
kukiuka vifungu vya Mkataba wa jumuiya hiyo.


Katika Maombi namba 6 ya kesi namba 9/2013 imefunguliwa na wanajumuiya hiyo Ally
Msangi,David Makata na John David Mbendo wanaowakilishwa na wakili
Jimmy Obedi wa kampuni ya Jimmy Obedi ya jijini Dar es salaam taarifa hiyo
imepokelewa leo na afisa masijala wa mahakama hiyo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwaniaba yamsajili.
Akiongea mbele ya waandishi wa habari wakili Obedi amesema wamewasilisha maombi hayo
ya kutaka maazimio yote ya vikao vilivyofanyika mnamo juni 24,25 mwaka huu huko
Entebe Uganda,kikao cha agosti 28,2013 Mombasa na kile cha oktoba 28,2013
Kigali Rwanda bila kushirikisha nchi mwanachama ambaye ni Tanzania.
“Lengo la maombi haya ni kuzuia utekelezaji wa maamuzi yaliyofikiwa
kwenye vikao hivyo kwa kuwa ni kinyume na vifungu vya mkataba wa
jumuiya,ibara ya 71(f)71(b) na vingine….hivyo tumeomba maombi hayo
yasikilizwe upande mmoja na kutoa uamuzi wa kusitisha utekelezaji
huo”amesema wakili.
Wakili huyo amesema wakati kesi hiyo ikisubiri kupangiwa jaji watu
wengine kutoka katika jumuiya hiyo wanaruhusiwa kujiunga na
walalamikaji hao ,kwa nia ya kuhakikisha mkataba wa shirikisho hilo
unafuatwa kwamujibu wa sheria.
“Hapa walalamikiwa ni wanasheria wakuu wanchi hizo tatu ambao Marais
wao wamekuwa wakikutana kinyume cha mkataba wa shirikisho la jumuiya
ya Afrika Mashariki….na sisi tunataka sauti ya kimahakama ya kusitisha
utekelezaji wa maazimio yao… mahakama ndio chombo kikuu kitakachotoa
tafsri si siasa tena…alibainisha wakili.

POSTED BY:www.info@dirayetu.blospot.com
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment