WAZIRI
wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Bw. Stephen Wassira
(pichani), amesema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar umejikita katika
misingi ya kidugu si utajiri.
Bw. Wassira aliyasema
hayo Mjini Dodoma juzi akizungumzia madai ya baadhi ya watu waliodai
Muungano uliopo uvunjike kwani una gharama kubwa na umeegemea upande
mmoja.
Alisema kuungana kwa
nchi hizo hakukutokana na utajiri wa nchi mojawapo bali ulifanywa na
waasisi kwa ajili ya ulinzi na usalama wa nchi hizo ndio maana umejikita
kindugu zaidi.
"Wanaodhani upande
mmoja unanyonywa, hawaitendei haki Tanzania ambayo imejikita katika
misingi ya undugu na kuzaa amani na utulivu uliodumu hadi sasa,"
alisema.
Alisema amani na
utulivu ni sehemu ya mafanikio ya Muungano ambapo wananchi wa nchi hizo,
wanafanya shughuli zao kwa amani, utulivu na ushirikiano mkubwa ndio
maana leo hii, kila Mtanzania ana haki ya kufanya shughuli zake eneo
lolote ilimradi havunji sheria au Katiba ya nchi.
"Huwezi kusema gharama
zinazotumika katika Muungano ni kero, tunapaswa kuangalia mambo kwa
misingi ya kujenga nchi si kubomoa, nawaomba baadhi ya wabunge wachunge
ulimi wao kwani nchi nyingi zimeingia katika machafuko kwa kauli kama
hizo," alisema.
Alikemea tabia ya
baadhi ya Watanzania wakiwemo wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kutoa
kauli zinazoweza kuwagawa wananchi kwani mataifa mengi duniani,
yanatamani Muungano uliopo.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment