Picha
ya chini na juu ni baadhi ya majeruhi walikuwa kwenye basi hilo aina ya
Urio lililopata ajali leo jioni katika eneo la Kia wilayani Hai mkoani
Kilimanjaro
wananchi
wawakiwa wanashuhudia ajali hiyo iliotokea leo jioni katika eneo la kia
ambapo inasemekana watu zaidi ya 31 wamejeruliwa
Basi
aina ya Urio lenye namba za usajili T 137 BCX linalofanya safari zake
moshi kuelekea leguruki mkoani Arusha leo limepinduka katika eneo la
kia na kujeruhi watu zaidi ya 31
kwa
mujibu wa mashuhuda waliokuwepo katika eneo la tukio walisema kuwa
dereva huyo alikuwa anajaribu kukwepa pikipiki iliyokuwa imejichomeka
barabarani
"dereva
huyu alikuwa anajaribu kukwepa pikipiki ndipo gari ikamshinda na kuama
barabara ndipo ilipo anguka gafla na kubiringita mara tatu apa yenyewe
unavyoiyona tumeigeza ilikuwa kichwa chini matairi juu"alisema mmoja
wapo wa shuhuda ambaye akutaka kutaja jina
mpaka
kamera ya libeneke la kaskazini inaondoka eneo la tukio watu 31 walikuwa
wamekwishwa pelekwa katika hospitali ya wilaya ya hai kwa ajili ya
matibabu wakiwemo wanafunzi wa shule ya leguruki ambao walikuwa
wanarejea shuleni mara baada ya kumaliza likizo yao ya sikukuu ya
pasaka
CHANZO LIBENEKE LA KASKAZINI
0 comments:
Post a Comment