Mjumbe
wa Bunge la Katiba, Mhe. Ezekiel Oluoch akiingia jana kwenye kikao
cha Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma. Mhe. Uluoch, ambaye pia ni naibu katibu mkuu wa Chama cha Walimu (CWT), ni mmoja wa wachangia mada wakubwa aliyejipatia umaarufu mkubwa mjengoni.
Mhe. Uluoch akisimama kutoa ufafanuzi kuwa yeye hana kundi bungeni humo.
Wakati
bunge Maalum la Katiba linaendelea na kikao leo, baadhi ya wajumbe
waliokuwa wanasemekana kuwa ni wanachama wa umoja wa kinachoitwa katiba
ya wananchi (UKAWA) wamejitokeza na baadhi yao kukanusha kuunga mkono
umoja huo. Mmoja
wao ni Mhe Ezekiel Oluoch ambaye alikuwa anadaiwa kuwa miongoni mwa
WANA UKAWA aliingia Bungeni jana na kukana kuhusika na umoja huo na
kuongeza kuwa yeye hana kundi lolote ndani ya bunge, na kwamba
ataendelea na kazi ya aliyoteuliwa kuifanya.
Mjumbe
ambaye ni mwakilishi wa wakulima Mhe.Hamisi Damumbaya akichangia
pamoja na kuwataka UKAWA kurejea kwenye mchakato wa katiba mpya.
Amewasifu viongozi wa dini kwa kutumia mahubiri kuelimisha wananchi
kuhusu katiba wakati wa kipindi cha ibada za Pasaka nchini kote.
Hii
inafuatia kikundi kinachojiita umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA)
kususia Bunge wiki iliyopita, na baada ya baadhi yao kurudi na kuendelea
na bunge kama kawaida.
Wanaoendelea
na bunge wengi ni kutoka kundi la wateule 201 na baadhi ya vyama vya
upinzani ambao mwanzo walionekana kuunga mkono UKAWA.
Na Deusdedit Moshi Mtendaji Mkuu wa
Photo Solutions Wawakilishi wa Michuzi Blog Kanda ya Kati.
0 comments:
Post a Comment